Breaking News: Waziri wa Kikwete Arudisha Hela za Escrow

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amerejesha Tsh 40.4 milioni alizopewa katika mgao wa fedha zilizochotwa kutoka akaunti ya Tegeta Escrow
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni vizuri anarudisha. Lakini isiishie hapa tukaona innocense ya watu hawa. Isingekuwa chama cha Chadema hii ilishaliwa, ilishagubikwa.Wamelindana wameona hapa haiwezekani tena. Na hii lazima itazamwe upya. Waziri asifahamu linalofanyika kumuana mtu anagawa mabillioni na anakesi. Angerudisha wakati ule na kusema angalau ahsante lakini kama waziri siwezi kupokea sababu ya tuhuma kubwa za ufisadi. Tusijisafishe kiurahisi na tukajipaka mafuta matakatifu hasa tukilinganisha na ukubwa wa jambo lenyewe, lilivyochezewa na viongozi wakuu wengi wa juu wa CCM. Kuna watu wamepoteza maisha kwa hili. Kuna watu waliwekwa ndani kwa hili sababu ya uwingi wa viongozi wa CCM bungeni ambao bado unaendelea.Kuna waliosaini hii mikataba, inabidi bila kinga wachukuliwe sheria za haki na ndipo tu tutaona ukweli, wa nia ya Raisi ndugu Magufuli analolifanya ni sahihi.Nani alijua ya kwamba Ngeleja atakuja kukiri na kurudisha pesa. Bado wako bungeni, bado wanatetea mambo mengine ambayo inabidi yakemewe na yabadilishwe na wachukuliwe hatua kali kuwapa moyo Watanzania kwamba nchi tunaibadili na hatutavumilia hii tena.Huku kuoneana huruma kama watoto wadogo wasiojua kitu halitapeleka Taifa hili mbele. Bado kutakuwa na chuki, hila, upendeleo, uhasama, unyanyasaji, ubabe, ufumbaji midomo, na mateso kwa wale waliosimama kidete kufumbua haya maovu.Ni wao sasa wananyanyaswa sasa. Na Watanzania wengi wenye akili wanaona haya mambo. Tanzania ya sasa wengi werevu, wanautambuzi. Inabidi serikali ielewe wengi wamefunguka macho na mnazidi kuwafungua macho. Ni ushindi kwa Watanzania kuona watu wanakiri wanarudisha pesa. Je mangapi mengine makubwa yamejificha? Cheo ni Dhamana. Umepewa Cheo si ujinufaishe. Tenda haki.

    ReplyDelete
  2. Wapi blog yangu Jamani. Hapa tunafundishana na kupeana mawazo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad