Chadema Yapata Pigo Jingine...Diwani Ahamia CCM


Diwani wa Ngabobo (Chadema), Solomon Laizer ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na CCM kwa maelezo kwamba anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Laizer ni diwani wa tano katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kutoa sababu kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Christopher Kazeri amethibitisha leo (Julai 11) kupata taarifa za kujiuzulu kwa Ngabobo.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema kujiuzulu kwa diwani huyo ni mchezo mchafu akidai  amenunuliwa.

Amesema tayari walipata taarifa za diwani huyo kushawishiwa kujiuzulu na kwamba, alifuatwa na viongozi wa wilaya na kanda wa chama hicho aliowaeleza kuwa ameshawishiwa.

“Baadaye alieleza hataondoka lakini naona wamefanikiwa kumshawishi, tunashangaa viongozi wa Serikali badala ya kufanya kazi za maendeleo wanafanya kazi za kushawishi madiwani wa upinzani kuhama,” amesema.

Hata hivyo, madiwani wanaohama wanapinga kuwa wameshawishiwa kufanya hivyo.

Hadi sasa madiwani watano wa Chadema waliojiuzulu ni Credo Kifukwe wa Kata ya Murieti jijini Arusha.

Wengine waliojiuzulu katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kata zao kwenye mabano ni Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unaweza kuunga bila kuhama. Humuoni Zitto mara nyingi anaunga anayoyaamini. Vibaraka hawa na usomi wa kubabaishia wanakuwa vibendera. Kikra finyu na kutamani madaraka bila hekima na akili tambuzi.wache waende hawajijui. Wstaona baadaye kwamba hawana uhuru, sababu hawaufahamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hayo yako, lakini pia hukatawi kufikiria unayofikiria

      Delete
  2. Kwenye ukweli fikiria badala ya kukurupuka kujibu na kujitetea. Si Tanzania tu kunaupinzani. Dunia nzima. inatokana na elimu, namna unavyoisi, (life style), imani. Sijawahi ona hamahama kama Tanzania. Labda kwa vile ni mpya watu wanayumbayumba badala ya kuzingatia kwa dhati ni nini wanakitafuta cha nguvu kikipatikana kiutawala kitabadili mwelekeo wa nchi. Wengi hawafikiri long term. Ni sasa. Na hii inahatari zake. Mpangilio wa miaka mingi na vizazi ukitaka kuboresha kunamisukosuko mingi unaipitia lazima uelewe hivi. Unajijengea, na kuwajengea vizazi ubira, urahisi kwa kufuata sheria safi zinazotawala nchi na zinazokubaliwa na wengi. Ndio maana mchakato wa katiba mpya ulitakiwa upitishwe kwanza kabla ya haya yote, Watu wakajua wanatawaliwa kupitia sheria safi. Sababu waliokwamisha nchi ni hawahawa viongozi wetu waliolipeleka pabaya Taifa kwa uongo, ubadhilifu, na ubinafsi. Haya ndiyo yaliyoingiza rushwa na ufujaji wa mali zetu za asili. Huwezi ukalitengeneza Taifa na kurudisha hadhi ya nchi bila ya kuwachukulia hatua wahusika wakuu ambao walisaine sheria mbovu na mikataba mibovu. Ukiwakingia migongo na maraisi wanaofuata hawawezi kufanya kazi zao kwa kufuata sheria eti unawaheshimu. Ni wahalifu sawa na wanaoondoa dhahabu na machikichia. Ndo wao wamesababisha kwa kukurupuka. Na katiba mya inaondoa hii kinga kusudi nao walazimike kutenda kazi kwa kufuata katiba au wakubali kiyama. Tanzania mnawahurumia viongozi wapotoshaji wenye kauki asali matendo ya kiuhujumu ndio maana hatuendelei na Watanzania wengi tumelala, hatuna ujuzi na elimu zenye werrevu, au sisi ni wajinga pia. Huwezi kulia kwa kuibiwa ukamkamata mwizi akajisafisha, na ukambariki aendelee. Hii haieleweki. Basi msiwachukulie hatua vinyasi vidogo. Muibaji simu anashambuliwa mpaka anakufa. Mpotishaji na mhujumu wa mabilioni msomi anasamehewa je ni picha gani hii.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad