CHIN Bees: Siwezi Kubadilisha Jina Kwa Sababu ya Chid Benz

Msanii wa Bongo Fleva, Chini Bees amesema hawezi kubadilisha jina ili kumkwepa Chid Benz.

Wiki iliyopita rapper Chid Benz alimtaka msanii huyo kubadili jina kwa sababu yanafanana kitu ambacho Chin Bees amekuja kukupinga.

“Mimi siwezi kubadilisha jina kwa sababu ya Chid Benz kwa sababu halifananini, very different. Mimi nafanya muziki wangu, siwezi nikakaa nipiganie jina, hivyo bro kama anahitaji jina dah!, sidhani kama jina langu linaendana na lake  me am do my thing,”  Chin Bees ameiambia E-News ya EATV.

Sababu ya Chid Benz kumtaka Chin Bees kubadili jina aliadai kwanza yamefanana na pili yeye ana hit song song 32 huku akiadai C. Bees hana hata nyimbo saba, hivyo hawafanani.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mambo mengine bana ni ya kipuuzi kweli mbona kule marekani wapo wanamuziki na pia ni waigizaji maarufu wa sinema wenye majina ya ICE T. na ICE CUBE na hatujawahi kusikia kuwa mmoja wao anadai eti mwenzake abadilishe la ICE mambo hayo ya kishamba utayaona bongo tu hasa kwa hao wanaojiona SUPER STARS ni balaa tupu kila kukicha ili wapate kiki za kipuuzi mtandaoni

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad