Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa Sh.5,000,000/=.
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa na watuhumiwa kuwapa rushwa ya Sh.10,000,000/=
Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo.
Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 wamepewa dhamana.
Mkuu wa TAKUKURU (M) Kinondoni Bi.T. MNJAGIRA anawaasa Viongozi wote wa Umma, Wanasiasa na Watumishi wote wa Serikali, kuheshimu nyadhifa zao na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria bila kujihusisha na vitendo vya Rushwa. Pia, anatoa wito kwa Wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria, Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumezuia vitendo hivyo visiendelee kujitokeza katika Jami