Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametuma salamu la rambirambi kufuatia kifo cha Waziri wa usalama wa Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery aliyefariki ghafla katika hospitali ya Karen iliyopo Nairobi muda mfupi baada ya kupelekwa kwa uchunguzi.
Meja Joseph Nkaissery alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla ya umauti kumkuta, Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Kenya Joseph Kinyua amethibitisha kutokea kwa kifo cha Waziri wa Ulinzi wa Kenya.
Baada ya taarifa hizo kusambaa Waziri Mstaafu Edward Lowassa amesema Nkaissery alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri na wakupigiwa mfano
"Natuma salamu zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri Joseph Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano, Mungu amumlaze mahali pema peponi" alisema Lowassa
Joseph Kasaine Ole Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka mwaka 2002 mpaka 2014 na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa Kenya mpaka kifo chake, mbali na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii ya Maasai nchini Kenya.
EDWARD Lowassa Aguswa na Kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya
0
July 08, 2017
Tags