Everton inafungulia Milango Tanzania - Mwakyembe

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema ujio wa timu ya Everton nchini utaweza kufungua fursa nyingi kwa kuwa dunia nzima sasa itaitazama Tanzania kupitia mchezo kirafiki dhidi ya Gor Mahia.


Mwakyembe amebainisha hayo muda mchache alipoupokea ugeni huo huku akizisisitizia timu za Tanzania kutumia viwanja vilivyopo nchini vizuri ili waweze kuinua vipaji kwa hali ya juu.
"Hii ni fursa kubwa kwa watanzania kwanza kuwaona hawa nyota wa Everton ni timu kongwe kutoka Uingereza lakini pili inafungua fursa sana maana inatutangaza watanzania kidunia, wamekuja na watangazaji kutoka nchi mbalimbali. Kwa hiyo inafungua milango kwa timu nyingi zaidi, nasi tuzishawishi zaidi timu zetu zije kutumia viwanja vyetu vya kisasa tulivyo navyo", amesema Mwakyembe.

Pamoja na hayo, Mwakyembe amewatuliza wanahabari pamoja na wapenzi wa soka kuwa na moyo wa uvumilivu kwa kuwa hawataweza kupata nafasi ya kukiona kikosi hicho kikiwa kinafanya mazoezi yake kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kutokana na kuwepo na ulinzi mkali.

"Nafikiri kesho kutakuwa na mchezo mzuri kweli, leo watafanya mazoezi katika uwanja Taifa lakini naona wenzetu hawataki kabisa kuona vyombo vya habari pale, hatuwezi kuwapinga kwa hilo. Kwa hiyo vijana wangu msihangaike hata kwenda pale maana kuna ulinzi mkali lakini kesho nitahakikisha kila mmoja wenu anapata nafasi nzuri kuweza kufuatilia mchezo huo jioni", amesisitiza Mwakyembe.

Everton itashuka dimbani kesho (Alhamis) kuchapana na Gor Mahia mchezo wa kirafiki baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa michuano ya Sportpesa Super Cup 2017.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad