FULL VIDEO: Mashtaka 7 Aliyosomewa Yusuf MANJI Akiwa Kitandani Hospitalini

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo July 5, 2017 ilihamia kwa muda katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kumsomea mashtaka saba ya uhujumu uchumi, mfanyabiashara maarufu Yusufu Manji na wenzake watatu.

Hatua ya Mahakama kuhamia JKCI ilikuja baada ya Manji kushindwa kuhudhuria Mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka hayo kutokana na kuugua na kulazwa katika Taasisi hiyo.

Jopo la Mawakili wa Serikali likiongozwa na Mutalemwa Kishenyi, Nassoro Katuga na Tulumanywa Majigo ilisomwa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

1: Kujipatia bidhaa isivyo halali

Mnamo June 30, 2017 katika maeneo ya Chang’ombe A Temeke DSM walikutwa na askari Polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zenye thamani ya Tsh. 192.5m ambazo zilipatikana isivyo halali.

2: Mabunda manane ya vitambaa

Wakili Majigo alidai kuwa washtakiwa hao walikutwa na Maofisa wa Polisi katika eneo la Chang’ombe A Temeke DSM wakiwa na bidhaa za mabunda manane ya vitambaa vya kutengrneza sare za JWTZ zenye thamani ya Tsh. 44m.

3: Kukutwa muhuru wa Serikali

June 30, 2017 Washtakiwa hao walikutwa na muhuri wa Serikali wa JWTZ isivyo halali ambao umeandikwa “Mkuu wa Kikosi 121 kikosi cha JWTZ” bila ya kuwa na uhalali na kwamba kitendo hicho kinahatarisha uchumi na Usalama wa nchi.

4: Kukutwa na muhuri wa Serikali

Katika shtaka la nne Washtakiwa wanadaiwa kukutwa na muhuri wa Serikali wa JWTZ isivyo halali ambao umeandikwa “Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupola Dodoma” bila kuwa na uhalali na kwamba kitendo hicho kingeweza kuhatarisha Usalama wa nchi.

5: Kukutwa na muhuri wa Serikali

Alidai, washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na muhuri wa serikali uliandikwa “Commanding Officer 835 KJ Mgambo, P.O. Box 224, Korogwe kinyume na sheria.

6: Mali iliyopatikana isivyo halali

Katika shtaka la sita, katika maeneo hayo hayo wanadaiwa kukutwa na Mali inayodhaniwa kupatikana isivyo halali ambayo ni namba ya gari zinazosomeka SU 383 mnamo July 1, 2017.

7: Kukutwa na Namba ya gari kinyume na sheria

Shtaka la saba ambalo washtakiwa hao wanakabiliwa nalo ni kukutwa na namba ya gari inayosomeka SM 8573, kinyume na sheria.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu mashtaka kwa sababu makosa hayo hapo chini ya Uhujumu Uchumi na Usalama wa Taifa huku upande wa mashtaka ukiwasilisha hati ya pingamizi la dhamana kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP).

Hii VIDEO ina kila kitu…bonyeza PLAY kutazama!!!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad