Picha A inaonesha jinsi watu wengi wanavyotumia vyoo vya kukaa wakiwa wanajisaidia haja kubwa. Wanasayansi wanasema kuwa mkao wa aina hii si sahihi kwakuwa unakunja utumbo na kufanya kiasi kikubwa cha uchafu kubaki tumboni.
Picha B ni jinsi utumbo unavyokunjwa kwa sababu ya kukaa kama inavyooneshwa kwenye picha A.
Picha C inaonesha mfano wa mtu anayejisaidia haja kubwa akiwa amechuchumaa. Hii ni aina ya asili ya kujisaidia haja kubwa ambapo utumbo haukunjwi. kwahiyo, wataalamu wanashauri kwamba hata unapotumia vyoo vya kukaa, inatakiwa mkao wako uendane na mkao wa asili wa kujisaidia haja kubwa (yaani uendane na kuchuchumaa).
Picha D inaonesha jinsi utumbo hasa sehemu ya mlango wa kutokea haja kubwa inavyokuwa ipo huru tofauti na inavyoonekana kwenye picha B
Kifupi, usahihi wa kujisaidi haja kubwa ni kama ifuatavyo:
1: Magoti yainuliwe juu zaidi ya mapaja
2: Inama mbele kidogo na uweke viwiko vya mikono magotini mwako
3: Tunisha tumbo lako na unyooshe (uti wa) mgongo