Timu ya taifa ya Tanzania ‘Tsifa Stars’ imeshindwa kupata ushindi kwenye mechi yake ya kwanza ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) itakayofanyika Kenya mwaka 2018.
Stars ilijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutanguliwa kufungwa goli la mapema dakika ya 17 kipindi cha kwanza na Dominique Nshuti.
Dakika ya 34 Himid Mao Mkami akaisawazishia Stars kwa mkwaju wa penati kufuatia beki wa Rwanda kuushika mpira kwenye penati box wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa hatari golini kwao.
Baada Stars kusawazisha bao, wachezaji wa Rwanda mara kadhaa walikua wakitumia mbinu ya kujiangusha ili kupoteza muda. Golikipa wa Rwanda Marcel Nzarora alikua kiongozi kaika zoezi la kuchelewesha muda hadi kupelekea kuoneshwa kadi ya njano.
Kocha wa Stars Salum Mayanga alilazimika kufanya mabadiliko kipindi cha kwanza baada ya beki wake wa kuli Shomari Kapombe kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kulazimika kupumzishwa. Boniface Maganga aliingia kuchukua nafasi ya Kapombe.
Wakati dakika zikiwa zimekaribia kumalizika, Mayanga alimpumzisha John Bocco na nafasi yake ikachukuliwa na Stamili Mbonde.
Stars itarudiana tena na Rwanda Julai 23, 2017 katika mchezo ambao utaamua ni timu gani itasonga mbele baada ya matokeo ya mwisho ya mchezo huo.