HOMA ya Ini Hatari zaidi ya UKIMWI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa homa ya Ini umetajwa kuwa ugonjwa hatari zaidi na wenye kuuwa watu wengi polepole, huku takwimu zikiwa zinaonyesha una maambukizo makubwa mara 10 kuliko

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
ya UKIMWI.

Mhe. Ummy amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari katika kilele cha maadhimisho ya siku ya homa ya Ini duniani yaliyofanyika leo.

"Nikiwa Waziri mwenye dhamana ninachotaka kuwaeleza Watanzania kwamba ugonjwa wa homa ya Ini umetajwa kuwa ugonjwa wa hatari na unaouwa watu wengi polepole. Kati ya watu 100, wanane wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa huo na mbaya zaidi wanaweza wasiweze kuonyesha dalili za ugonjwa", amesema Ummy.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy ameendelea kwa kusema "kwa mara ya kwanza ugonjwa huu unapewa kipaumbele unaostahili na kupitishwa na Shirika la Afya duniani katika mpango mkakati wa kwanza wa homa ya ini na kuanza kufanya kazi kuanzia mwaka 2016 mpaka 2021. Sisi serikali ya Tanzania tumekubali mkakati huu wa kwanza kwa maana tunataka kutokomeza kabisa ugonjwa huu", amesema Ummy.

Kwa upande mwingine, Ummy amesema kati ya watu laki mbili mwaka jana (2016) waliochangia damu, asilimia sita wamekutwa na maambukizi ya virusi vinavyosababisha homa ya Ini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad