Huku Jamali Malinzi Akiendelea Kusota Selo...TFF Yamchagua Huyu Kuwa Kaimu Wake

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imekutana jana Jumamosi Julai 01, 2017 kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam imempitisha Wallace Karia kuwa Kaimu Rais wa shirikisho hilo huku Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi kuwa Kaimu.

Viongozi hao watakaimu nafasi tajwa hapo juu hadi mahakama itakapotoa maamuzi kuhusu kesi zinazowakabili kwa sasa ambaye ni  Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine.

Kamati ya Utendaji ya TFF, imekutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6) na kufanya uamuzi huo.

Katika hatua nyingine, Karia amesema ujumbe wa FIFA unakuja nchini kufuatilia sakata zima la viongozi hao wa TFF kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad