Baada ya tetesi nyingi kuhusu ujio wa iPhone 8 wengi wakihoji muonekano wake utakuwaje na sifa nyingine tayari wataalamu wa teknolojia wameshavujisha muonekano wa simu hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na watumiaji wa simu hizo na inatarajiwa kutoka Septemba mwaka huu.
</
Video inayoonesha muonekano wa simu hiyo imevujishwa na mtandao wa stevehemmerstoffer.com na inaonesha muonekano wa simu hiyo vizuri kabisa ambapo unakupa nafasi ya kuhakiki baadhi ya sifa ambazo awali zilikua ni tetesi tu kutoka kwenye mitandao mingine duniani.
Kupitia video hiyo Kampuni ya Apple Inc inaonesha wameongeza kioo cha simu hiyo ikiwa ni pamoja na kuficha button ya katikati kwenye kioo ambapo inasemekana pia fingerprint sasa itakuwa kwenye kioo.
Kwa upande wa ukubwa wa simu hiyo video inaonesha itakuwa na urefu wa 137mm na upana wa 67.5mm ikiwa na tofauti ndogo na vipimo vya toleo lao la iPhone 7.
Sifa nyingine itakuwa na Wireless Charger, Camera ya mbele na Home Button zitakuwa kwenye kioo (Display), Kamera ya nyuma itakuwa na Mega Pixel 12 na ya mbele Mega Pixel 8 na gharama yake itakuwa ni zaidi ya dola $1000 sawa na Tsh milioni 2.2 kutegemeana na ukubwa wa simu.
Je, mdau wa simu za kampuni hiyo pendwa kabisa duniani umeupokeaji ujio wa simu hii? na muonekano wake unauonaje?