HUYU Ndiye mh. Freeman Mbowe Kiongozi wa Chama cha Upinzani (CHADEMA) Nchini Tanzania Ninayemkubali

(1) Aliipasua CCM vipande vipande mwaka 2015 kwa kumfanya Lowasa kuwa Mgombea kiti cha Urais na kuufanya uchaguzi kuwa mgumu ktk historia ya nchi ya Tanzania Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya Kisiasa mwaka 1992.

Wafuasi wa CCM mamilioni waliamia CHADEMA na kwa tafiti za awali tu zinaonyesha bado wana hali ya kuja kumpigia kura za kutosha Lowassa mwaka 2020 na inaonyesha wengine watazidi kuiunga mkono CHADEMA maelfu ya wasomi Kutokana na kuitazama nchi kwa jicho la Tatu.

(2) Ndiye aliyekilinda Chama Cha Demokrasia Maendeleo(CHADEMA) kuwa chama Tishio kwa Chama Tawala (CCM). Vyama vingi vya upinzani Barani Afrika viliingiziwa vibaraka wa kisiasa na kuviharibu lakini si kwa CHADEMA ,,,mamluki na vibaraka huhama wenyewe au huumbuka kabla ya njama zao kutekelezeka na hatimaye kutimuliwa mapema .

(3) Ndiye kiongozi ambaye hanunuliki ,,hawezi kuwa kibaraka ndani ya mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania.Wanasiasa wengi wa Afrika hususani wa upinzani ni wanafiki na wasaliti huweza kununulika na vyama Tawala lakini si kwa nguli huyu wa siasa nchini Tanzania.

(4) Ndiye kiongozi anayetafutiwa kashifa ili akose credits za kuongoza CHADEMA na Taifa lakini imeshindikana. Mkumbuke kashfa za madawa ya kulevya . Ile kashifa ipo wapi ? Ikumbuke iliibua taharuki kubwa lakini sijaisikia tena.ILIPOTEA kama upepo .

(5) Ndiye kiongozi aliyewaandaa viongozi wengi wajao watakaopambana na Dhuluma na maonevu ndani ya Nchi mpaka nje ya mipaka ya Nchi .
Nikiwa kwenye Taasisi za Elimu ya juu mbalimbali nilishuhudia vijana wakipokea kweli zake kisiasa na kuwa wakakamavu wa hoja kupitia mikutano yake ya Kisiasa hususani anapofanya mikutano ya waandishi wa habari(Press conference ) kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na anapozungumza bungeni .

Kweli zake zimefanya wasomi wengi kufanya CHADEMA kuwa jukwaa halisi na la kuaminiwa ktk kuyazungumzia masuala ya Kitaifa hususani yanayolenga kuliondoa Taifa lilipokwamia mfano Kuwaletea wananchi wa Tanzania Maendeleo na kupigania haki zao dhidi wale wote wakandamizaji wa haki .

Kama mnasema Rais Magufuli ni mpigania haki za watanzania mnapaswa kujua kabla hajawepo Magufuli basi CHADEMA ulikuwepo na ndio imeibua kashifa zote za Mafisadi na wala Rushwa Serikalini bila kusahau Biashara ya madawa ya kulevya .

CHADEMA ikishirikiana na CUF ,NCCR mageuzi na wadau wa kupambana na Ufisadi iliibua kashifa za Mabehewa na vichwa vya Treni vibovu ,kashifa ya RADAR,MEREMETA ,ESCROW n.k .Kashifa zote Zilisimamiwa na kujadiliwa vilivyo chini ya Captain Mbowe akiwa kiongozi mkuu wa vyama vya upinzani Bungeni.

(6) Ndiye aliyefanya kila mtanzania kwa asilimia kubwa kuwa Mwanasiasa na mwanaharakati na kuweza kupaza sauti dhidi ya wala rushwa na mafisadi .CCM kiujumla wanaweza kukataa lakini kuna wafuasi wengi wa CCM wamejifunzia kwa Mbowe ujasiri wa kusema ukweli juu ya Ufisadi na wizi wa fedha za Umma ulikuwa unaendelea Serikalini mfano masuala ya ESCROW, RICHMOND, Kashifa ya RADAR, Mishahara hewa,Wafanyakazi Hewa,Usafirishaji wa wanyama Hai nje ya Nchi n.k

(7) Ndiye kiongozi mvumilivu kisiasa Barani Afrika.Mara nyingi kauli zake zimeleta Mshikamano wa kitaifa badala ya kuleta matengano ya kitaifa. Hatakama kaonewa kajitahidi kuwa mwenye Hekima na Busara ktk kutetea haki zake .

(8) Ni mtu anayeitazama Tanzania kwanza badala ya CHADEMA. Ni mtu anayetazama watanzania kwanza kabla ya CHADEMA. Ni mtu wa mikakati kuliko maneno. Ni Simba wa mikakati ya kisiasa na kuthibitisha hilo Mtaona 2019-2020 mwaka 2015 mlishuhudia .

Mh.Freeman Mbowe kwa mwenye Akili Timamu hawezimpuuza hata Mara moja hususani ktk kuleta mageuzi MAKUBWA ya kiuchumi ,Kisiasa na kijamii . Kwa jamii ya kistaarabu na watu wasio na upendeleo Mbowe hapaswi kupuuzwa. Yote Niliyotaja HAPO juu Yana umuhimu mkubwa sana kwa Taifa letu.

Lakini nitaeleza umuhimu wa matukio au mambo mawili kwa kuwa mengine tajwa yamejieleza kiundani . Umuhimu nitakaoeleza ni wa matukio mawili ambayo ni kitendo cha kuigawa CCM vipandevipande na kitendo cha Mbowe kuilinda CHADEMA isiingiliwe na CCM . Twende pamoja ktk kuelezea umuhimu wa matukio hayo mawili,,,,,,,

(1) Kitendo cha Mbowe kuigawa CCM vipandevipande kwa kukubali Lowassa atumie jukwaa la kisiasa la CHADEMA kuwa mgombea Urais mwaka 2015 kuliifanya CCM ianze kujikagua na kuanza kujibadilisha mienendo yake kupitia baadhi ya viongozi wake na watendaji wa serikali Kuifanya nchi ya Tanzania kuwa shamba la bibi.

CCM ilijisahau sana HAPO hapana ubishi ,,,CCM iliamini Kuwa watatawala milele bila shaka 2015 waliamini sasa kwamba IPO siku watang'oka wakiendekeza mambo ambayo wananchi wa Tanzania hawayataki .Nakumbuka mwaka 2014 katibu mkuu wa CCM mh.Abuldulhaman Kinana aliwahi sema kuna mawaziri mizigo ktk Serikali ya awamu ya nne ,,,

sasa mawaziri hao hawa kuwa ni mizigo kwa maana ya vifurushi no walikuwa na kashifa nyingi za Ufisadi na wizi wa fedha za walipakodi masikini wa nchi hiii na kuna mawaziri wengine walisaini mikataba isiyo na tija kwa Taifa bila shaka walisaini kwa faida zao wao wenyewe.

(2)Kitendo cha MBOWE kuilinda CHADEMA isiigiliwe na CCM kama chama Tawala kumekifanya chama cha CHADEMA kuwa kioo cha kujitazamia kwa CCM na Serikali yake kwa miaka takribani 25 ya mfumo wa vyama vingi nchini tokea mwaka 1992 ,,,kwa maana ya kwamba ili CCM ijue imekosea au imepatia lazima itumie CHADEMA kama kioo chake cha kujitazamia ,,,,,na ndio kazi kubwa ya chama cha upinzani chochote chenye nguvu ktk nchi ya kidemokrasia.

Kauli ya Rais Magufuli ya hivi karibuni kwamba "Ukiona adui yako anakushangilia sana na kukusifu ujue umekosea na ukiona anakushambulia sana ujue umepatia''' inaonyesha wazi kuwa CHADEMA ni kioo kwa CCM na CCM inapaswa kuheshimu kioo hiki cha heshima Siyo kukiharibu .

Kioo cha kujitazamia ukikiharibu kuna wakati unaweza ukaenda nje ukadhani USO wako upo vizuri kumbe umebabuka ukatia aibu kwa watu nje.Kukipoteza chama cha CHADEMA ni faida kwa CCM na hasara kwa kitaifa kwani litakuwa likitembea gizani bila kujua nini kinaendelea ndani ya Serikali.

Daima nitasema kweli ,,Unafiki nitauweka kando kwa kuwa yapo maisha baada ya haya Duniani.

#CHADEMA #haiwezi #potea kwa kuondoka kwa Madiwani wenye njaa.

#Kutaka kupoteza #CHADEMA hakutaleta Maendeleo nchini Tanzania Bali ubunifu na utawala bora utaleta Maendeleo nchini.

#CHADEMA haijipotezwa hata wabunge
kununulika waacheni mamluki waende kwao.

#Ukweli haufi ,,uongo hufa.

Mwanahabari Huru

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 1)Lowasa alihama CCM si kwa ushawishi wa Mbowe bali kwa uroho wake wa madaraka (2)Mwenyekiti Mbowe ni kiongozi gani wa mfano anaeukumbatia ukanda? (3) Ni juzi tu tumesikia Chadema wakiongozwa na mwanasheria wao Tundu Lisu wakileta hoja fake ya udikteta zidi ya serikali wakati hoja za ukweli za udikteta na dikteta halisi kabisa ni mwenyekiti Mbowe. Yeye Mbowe ni mwenye kiti wa Chadema wa maisha. Na ndio maana alikubali kununuliwa na Lowasa ili amuzie nafasi ya kugombea uraisi sasa hao wanaosema Mbowe ni mtu asie nunulika ni wagonjwa wa akili. Kama demokrasia ingetendeka ndani ya Chadema na Dk salaa akapita kugombea uraisi basi hii leo kuna uwezekano mkubwa nchi hii kuwa chini ya serikali ya Chadema. Udhaifu Mkubwa wa mbowe ni kuwa na mawazo ya kiuwana harakati katika kukabiliana na changa zinazoletwa na serikali iliopo madarakani na kwa stahili hiyo lazima atafeli kwani serikali ni serikali mfano mzuri Marekani Democrats tangu kwisha uchaguzi uliomuweka Donald Trump wa Republican madarakani wamekuwa wakimpiga vita kila kukicha na kulalamika chini chini yakuwa uchaguzi hakuwa halali kwa kudai Trump ni kibaraka wa urusi lakini ukweli ni kwamba Democrats walipigwa kihalali kabisa na takwimu zilizotoka hivi sasa inaonyesha Trump anafanya vizuri sana kwenye uchumi kinyume na ilivuotararajiwa na wataalamu wa mambo ya siasa wameionya Democrats kuachana kabisa na uwana harakati zidi ya serikali ya Trump kwani wamerekani wengi wameanza kuamini yakwamba takribani ya miezi saba sasa wapinzani wa Trump hawana sera isipokuwa kumuandama Trump na kutokana na hilo watu wa siasa wanasema kuna uwezekano mkubwa chama cha Trump kikaibuka mshindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge ujao kama Democrats hawatobadilika. Huo ni mfano tu yakwamba actions always sound louder than words and Maghuful actions are speaking and sounding clear and louder than the opposition noise.

    ReplyDelete
  2. Ahaaa....!!! Bilikana na kina Choggy Slay..Nasikia imepotea!! Inakuwaje sasa.
    Deali ni Posho Dom. Au Vipi?
    Siasa ni magumashi tu!! Nunua VXR unaitwa Muheshimiwa hata kama ?Hujiheshimu. Si una xvr? Poa
    Mie yangu Macho na Jembe langu Magu!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad