Jamali Malinzi Aipasua Kamati ya Uchaguzi TFF... Kamati Yataka Malinzi Apitishwe Bila Kuwepo

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Revocatus Kuuli amesema yuko tayari kujiuzuru baada ya kutofautiana na wajumbe wake juu ya hatma ya rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ina wajumbe watano kati ya hao watatu na makamu mwenyekiti Domina Madeli wanataka Malinzi apitishwe bila ya kuwepo jambo linalopingwa na mwenyekiti Kuuli .

Katika usahili huo wagombea 70 wamepitishwa kati ya 72, lakini ilipofika wakati wa kujadili jina la Malinzi ndipo wajumbe walipotofautina.

Akizungumza baada ya kuvunja kikao hicho Kuuli alisema usahili ulienda vizuri kwa wagombea wote, uamuzi wa kutumika busara kwa rais Malinzi umesababisha kutoelewana kwa wajumbe na kusababisha amvunja kikao hicho hadi kesho, Jumapili.

Kuuli alisema baadhi ya wajumbe wametaka busara itumike kwa wagombea ambao hawapo yaani Malinzi kuwa apitishwe hata kama hayupo na vielelezo vyake viletwe na mtu mwingine.

Kuuli alisema anaheshimu mawazo ya wenzake ila  dhamira yake inamtuma kusimamia ukweli.

"Mtu hawezi kupitishwa wakati hakuwepo katika usahili na huo ndiyo msimamo wangu na kesho (leo) litaendelea kujadiliwa katika kikao hiki.

"Tukishindwana basi mimi nitajiuzuru kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF kwa sababu nina kazi nyingine za kufanya," alisema  Kuuli.

Makamu mwenyekitia Madeli alisema kwanza mwenyekiti hakai Dar es Salaam na vikao  vingi wamekuwa wakifanya uamuzi bila yeye kuwepo sasa kwa nini apige hii.

Madeli aliongeza kuwa kanuni haisemi kama usahili ni lazima uwe ana kwa ana.

WAPITISHWA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TWFA

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu mkoani Morogoro.

Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia

Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.

Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad