Je Kuna Ukweli Teuzi za Magufuli ni za Ubaguzi wa Kikanda?

Nimemsikiliza Mh Tundu Lissu jana, mbunge na mwanasheria wa chadema, akilalamika kuwa teuzi za mtukufu Rais ni za kikanda.

Mheshimiwa Lissu alidai kwa kueleza teuzi nyeti za serikali kuwa ni za kibaguzi na hazileti picha ya kitaifa.

Lissu aliwataja watu wafuatao kuwa wanatoka kanda ya ziwa.
1. Mwanasheria mkuu
2. Mkuu wa JWTZ
3.IGP
4.Mkuu wa usalama wa taifa
5.Katibu wa fedha na naibu wake
6. Katibu mkuu

Lakiki Lissu hakuangalia nafasi nyingine nyingi ambazo Rais ameteua watu ambao sio kanda ya ziwa, mfano
1. Baraza la mawaziri, 
2. Wakuu wa mikoa wanatoka kila kanda
3. Waziri mkuu
4. wakuu wa wilaya

Bado hoja ya Lissu inahitaji kujadiliwa ili kuweza kubaini ukweli wa jambo hili vinginenvyo etaleta sinto faham nyingi sana kiasi cha watu kushangaa mbona Rais hazindui miradi katika mikoa ya kaskazini.

Hatuwezi kuacha hili jambo kuelea, nilazima Lissu ajibiwe kwa ushahidi aondoe hii dhana potofu.

General Mangi/Jamii Forums
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ajibiwe Lisu kwa point ipi? Mikoa ya kanda ya ziwa na miaka mingi wamekuwa wakifanywa wasindikizaji katika masuala ya uongozi wa nchi yetu. Na ni ukweli usiopingika wananchi wa mikoa ya kanada ya ziwa wengi wao ni wachapa kazi, waaminifu na wenye elimu nzuri vile vile kuliko sehemu nyingi za tanzania. Wala haishangazi chadema kuzua kete ya ukanda kwani chama hicho kimeundwa katika misingi hiyo ya kibaguzi. Chadema hivi sasa wanatapatapa sawa na mfa maji anapojaribu kuyakamata maji. Chadema wameshindwa kisera,kisiasa nakadhalika na CCM haishangazi kuona wakijua na hoja za kipumbavu ya kujaribu kuwagawa watanzania. Na sera ya (Divide and rule) ni sera ya kikoloni walioitumia kuwagawa waafrica ili wawatawale sasa hapo utaona jinsi gani chadema walivyoishiwa. Na La lazima hapa la kujadiliwa hapa ni kwanini Chadema cha kikanda zaidi katika siasa za tanzania na sio iteuzi wa watanzania wachapa kazi kwa maslahi ya tanzania sio kwa maslahi ya kikanda kama wanasiasa wa hovyo wanavyotaka kutuaminisha ?

    ReplyDelete
  2. Ajibiwe Lisu kwa point ipi? Mikoa ya kanda ya ziwa na miaka mingi wamekuwa wakifanywa wasindikizaji katika masuala ya uongozi wa nchi yetu. Na ni ukweli usiopingika wananchi wa mikoa ya kanada ya ziwa wengi wao ni wachapa kazi, waaminifu na wenye elimu nzuri vile vile kuliko sehemu nyingi za tanzania. Wala haishangazi chadema kuzua kete ya ukanda kwani chama hicho kimeundwa katika misingi hiyo ya kibaguzi. Chadema hivi sasa wanatapatapa sawa na mfa maji anapojaribu kuyakamata maji. Chadema wameshindwa kisera,kisiasa nakadhalika na CCM haishangazi kuona wakija na hoja za kipumbavu ya kujaribu kuwagawa watanzania. Na sera ya (Divide and rule) ni sera ya kikoloni walioitumia kuwagawa waafrica ili wawatawale sasa hapo utaona jinsi gani chadema walivyoishiwa. Na La lazima hapa la kujadiliwa hapa ni kwanini Chadema ni chama cha kikanda zaidi katika siasa za tanzania na sio kujadili uteuzi wa watanzania wachapa kazi kwa maslahi ya tanzania sio kwa maslahi ya kikanda kama wanasiasa wa hovyo wanavyotaka kutuaminisha ?

    ReplyDelete
  3. HEBU JIANGALIENI NYINYI CHADEMA, NI HOJA ISIOKUWA NA MASHIKO,

    ReplyDelete
    Replies
    1. wanasema anatekeleza ilani ya chama chao sasa inakuwaje tena?

      Delete
  4. mnanikumbusha mbali sana.sizitaki mbichi hizi.

    ReplyDelete
  5. hili dubwasha linakurupukaga ili lisikike

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad