JE ni Utumuaji Vibaya wa 'MAMLAKA' Tanzania?

Kukamatwa kwa Mbunge wa upinzani nchini Tanzania Halima Mdee kwa madai ya kumtusi Rais John Magufuli kumeshutumiwa pakubwa huku wakosoaji wakisema kuwa ni ishara ya hivi karibuni kwamba serikali inatumia mamlaka yake vibaya ili kukandamiza uhuru wa kujieleza.

Msemaji wa chama cha upinzani CHADEMA, Tumaini Makene ameambia BBC kwamba chama hicho kitakwenda mahakamani dhidi ya hatua ya mkuu wa Wilaya ambae aliagiza kukamatwa kwake pamoja na makamishna wengine wote wanaokiuka sheria.

Bi Mdee ni mwanachama wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani katika Taifa hilo la Afrika Mashariki akipanda gari la polisi


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee aliyewekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Wilaya
Alituhumiwa na Ally Hapi, mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kumtusi Rais na kuchochea ghasia baada ya kudai kwamba Rais anafikiri kwamba matamshi yake ni Sheria na kwamba siku moja atawaagiza Watanzania kukaa utupu.

Muungano wa mabadiliko na uwazi unaongozwa na Zitto Kabwe ulisema kuwa hatua hiyo ni uendelevu wa utumiaji mbaya wa mamlaka.

”Sheria inayompatia mkuu huyo wa Wilaya uwezo wa kuagiza kukamatwa kwa mtu, hailingani na sababu ya kukamatwa kwa bi Mdee,” alisema.



Watu kadhaa wamekamatwa katika siku za nyuma kwa kuchapisha ujumbe katika mitandao ya kijamii ambayo mamlaka inadai inaingilia kisiasa.

Mamlaka inaamini kwamba inafuata sheria na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba hakuna ”migogoro yoyote miongoni mwa wananchi” nchini Tanzania.

Bwana Magufuli alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2015 na licha ya kukosolewa na upinzani pamoja na makundi ya wanaharakati anaungwa mkono na Watanzania wengi.

HT @ BBC Swahili
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Anaungwa mkono na wengi wasio na elimu.si wasomi weleve na watu wansojua sheria. Ni hatari sana kwa nchi eti kupendwa na watu ambao hawajui sheria za nchi.zamani shule zilifunfisha siasa , sheria na ujasiri. Pia taifa lilitoa elimu kwa vijana namna ya kulilinda na kulitetea taifa letu. Kwa miaka 15 sasa elimu imeshuka. Na kwa miaka hii serikali imetumia madaraka vibaya, imeliingiza Taifa kwenye hii mikataba mibovu cnini ya utawala wa chama tawala. Ni upinzani ambao umepigania kila siku kwa hali na msli kuirudia mikataba upya, imepigania vikali kwamba bunge lipate nguvu kuisoma mikataba. Ccm kwa miaka yote hii imekataa.nashangaa leo uvccm inajipongeza na kuchukua difa ambazo hawastahili, ni wao ndio waliohudika miaka yote hii, leo inachukua sifa isiyo ya kwao kugeuza kibao sababu tu rsidi katoka ccm wsnapata nguvu kutukana wapinzsni, kunyanyasa viongozi wa kipinzani na wote ambao hawaendani kifikra wanaswekwa nfani bila kufuata sheria. Kila mkuu wa mkoa, wilaya, na wabunge wa ccm wamepewa vibsli kunyanyasa, kufunga watu bila kufuata sheria. ni unysnyasaji mkubwa unaorudisha maendeleo ya watanzania wasomi nyuma na kumpa cheo mtu asiye na elimu ambspo inafanya ujingavutawale Taifa na ni aibu kubwa duniani. Hawa viongozi eote wahujumu ni wanachama wa ccm. Mnajua hili vijana wa taifa hili? Asilimia 99ya wahujumu eote ni watu wa madaraka ya juu na ni wanachama wa ccm ambao wslikuwa wsbunge, mawaziri, watu wa ikulu na ndugu zao na marafiki wa karibu..nawashangaa sana wanaounga mkono na kuona wapinzani kunysnyaswa ambao kwa miaka zaidi ya 15 wamelalamikia serikali kuhusu uhujumu na wizi wa mali za umma, na upendelea kwa wawekezsji na kukandamiza watanzsnia na kuwanyima hski zao.wangedikiliza wapinzani hii haingetokea hata.ni upurukushani na uzembe wa wanaccm umeangamiza mali za umma. Na bado hamruhusu wapinzani wsliolilia sheria kushiriki kuweka sheria safi na kulikomboa taifa. Hili swala linahusu watanzania wote hstuwezi kuwaamini ccm pekee smbao wao ni wahusika wakuu kwa huu ufujaji wa mali za watanzanis. Ondoeni vikwazo washirikisheni wspinzani ambao wameleta hoja hizi ili nchi itende haki kwa watanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad