KUISHIWA nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi hasa wenye umri mkubwa. Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndiyo wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo.
Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume. Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu. Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo hili.
Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani yaani testicles kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii au mbegu za kiume.
Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi, matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika zote.
Vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni;Umri wa mgonjwa, jumla ya afya aliyonayo kwa sasa, utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa, migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi nk.
TIBA Ni muhimu wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako, kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya tatizo linalokukabili, nenda akakupime na anaweza kukupa dawa kama ataona inafaa. Kwa ushauri wa bure piga au tuma ujumbe namba zilizopo hapo juu.