Jinsi Historia Inavyopinga MBOWE Kuwa Mtetezi wa Wanyonge

Mimi ni muumini wa Historia ya ukombozi, ninafahamu dunia nzima namna nchi zilizohitaji ukombozi namna zilivyopata ukombozi na namna ya viongozi wao waliowakomboa walivyojitokeza kwenye jamii.

Mbowe ndio mfanyabiashara pekee anayejiita mtetezi wa masikini duniani, tangu nimewahi kuifahamu historia ya ukombozi,

Hakujawahi kutokea Duniani labda ahera, Masikini wakatetewa na Tajiri, Haijawahi na Jaitawahi kutokea Mfanya biashara yoyote akapanga kupata hasarfa eti kwa maslahi ya Umma, wafanya biashara wote wanawaza faida, hata mbowe anawaza faida na sasa anatafuta faida kwa gharama yoyote.

Tunamsifia Mandela leo, Mandela hakuwa mfanyabiashara, Mandela hakuwa tajiri, Mandela alichangiwa na masikini wenzake kuikomboa Arika ya Kusini, Mandela hakuwahi Kuikopesha ANC pesa ili iwaondoe Makaburuu, Mandela alifanana na jamii aliyotaka kuikomboa na Mandela alifanikiwa kuikomboa.

Wote tunamsifia Nyerere Hapa Tanzania, Nyerere Hakuwa Mfanyabiashara, mwalimu Hakuwa Tajiri, mwalimu Hakuwahi kuikopesha TANU ili kumuondoa MKOLONI, nyerere alichangiwa na masikini wenzake, aliombewa na walalhoi wenzake na alilindwa na mafukara wenzake.

Mifano ni mingi, hivyo hivyo kwa Samora Machel, Kwame Nkuruma, Milton Obote, Robert Mugabe, Kamuzu Banda, Dkt Martin Lutherking, Mahatma Gandh, Mao Zedong, AmilicaCabra na wengineo wote, KAMWE KUNGURU WASIOFANANA HAWAWEZI KURUKA PAMOJA.
Nitaendelea kuwafundisha mengi ninayoyajua kuhusu MBOWE NA CHADEMA kwa kadri itakavyowezekana.

Jamii Forums

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hujui Mao Tse Tong alikuwa ni kiongozi wa namna gani kwa China niliwahi kuiona documentary film ya maisha ya Mao Tse Tong kwenye TV program moja hapa Ujerumani inayoitwa ARTE sikuyaamini macho yangu niliyoyaona humo kuhusu yeye akiwa kabla ya kuwa Rais na baada ya kuwa Rais na jinsi alivyowaua mamilioni ya wananchi wake katika utawala wake wenye mfumo wa kikomunisti aliishi maisha ya kibepari anasa pombe na sigara kwa wingi (he was a chain smoker)na muharibifu wa mabinti wadogo wadogo kwenye palace yake magari ya thamani toka ulaya ya magharibi kama Mercedes Benz wakati yaani huwezi kuamini jinsi alivyojijengea jina lake nje ya China lakini ni ukweli ya kwamba alikuwa pia kiongozi mwenye tamaa ya kujilimbikizia mali kwa hiyo katika list yako ya viongozi masikini kama wananchi wa chini mtoe kabisa Mao Tse Tong kwenye orodha yako

    ReplyDelete
  2. NDUGU YANGU LEONIDAS UMESEMA KWELI KABISA...UONGOZI KWETU HAPA NYUMBANI IMEKUWA NDO KITEGAUCHUMI MIE SIJAWAHI KUSIKIA ENZI ZILE MBOWE AKIMILIKI BILLS HATA WAKATI WA MBOWE AKITOA MISAADA KWA MASIKINI AU MAYATIMA..HOW COME SASA HIVI ANATUMIA MSEMO WA MTETEZI WA WANYONGE, WHERE WERE YOU ALL THOSE YEARS. ..
    WATU HAPA DUNIANI HATUMUOGOPI MUNGU NA TUMESAHAU UMAUTI KUWA NDO NJIA YA KWENDA KTK HUKUMU (MAHAKAMA YA MWISHO...WATANZANIA TUACHE TAMAA ROHO MBAYA NA CHUKI BINAFSI. .NI MIE LADY AHLAM

    ReplyDelete
  3. Wewe unaesema uliiona filamu ya Mao tseng wa china akinyanyasa watu wake ukiwa ujerumani huna akili pengine unaukosefu wa elimu dunia. Kwa kukuelimisha tu nchi zote za kibepari zimekula kiapo cha kuingamiza mifumo yeyote ile ya kimaisha inayofuatwa na chi za dunia isipokuwa uperi. Na katika hilo si ajabu ukiwa uingereza,ujerumani, Marekani,ufaransa nk kuona wakipropanda maovu kwa viongozi waliowakatalia kuwaabudu. Mfano wajuremani kihistoria hawana haki ya namna yoyote ile ya kumnyoshea kidole mtu au kiongozi yeyote aliepita kwa maovu, wanatakiwa kutubu mpaka kiama. Marekani zaidi ya watu million moja na zaidi waliuwawa katika vita vya kuwalazimisha watu fulani kufuata matakwa ya watu fulani lakini hujawahi kusikia kiongozi wa vita hiyo akilaniwa kwa mauaji kwa kuwa.. Marekani. Kila nchi inahistoria yake na kwa kila kiongozi wa zama hizo walitumia nguvu za ziada kuwaunganisha watu wao kulingana na mazingira waliyokuwa wakikabiliana nayo lakini wazungu ndio waliokuwa watu makatili kuliko watu wa mataifa mengine licha ya kujivisha joho la binaadamu mwenye huruma zaidi kuliko wengine .

    ReplyDelete
  4. Kamwe MBOWE hawezi kuwa mtetezi wa wanyonge, kama aliweza kukwepa kodi miaka 20 hafai hata kuwa kiongozi huko ni kuwaibia wananchi, pia ni mnafiki mkubwa, kwa tunaokumbuka, alidiriki kusema kuwa ANAWASHANGAA WANAOCHOMA VIBAKA NA KUMUACHA LOWASSA AKIKAMUA MITAANI, lakini yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumpokea alipotemwa na CCM. Awadanganye wenye upofu wa mawazo. Watanzania wa sasa wanajuwa Mchele upi na Chuya zipi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad