JUA Aina ya Watu Wasionuka Vikwapa Wala Kuitaji Kutumia Deodorant......

Je wewe ni miongoni mwa wachache wenye bahati hii?

Kwa jinsi joto linavyoongezeka na msimu wa kiangazi ukiwa unakaribia, wengi wetu tunafikiria jinsi ya kukabiliana na kutoka jasho na harufu inayoambatana nayo. Lakini kama wewe ni miongoni mwa watu wachache wenye bahati zao ambaye una vinasaba (DNA) vinavyoitwa ABCC11, huna haja ya kuwa ma wasiwasi wa kutafuta deodorant ilipo.

Kwa mujibu wa tovuti ya LiveScience, uwepo wa kinasaba hicho inamaanisha kwamba vinyweleo vyako vya makwapa vinakosa kemikali ambayo ikichanganyika na jasho kinakuwa chakula cha bakteria na mwisho kutengeneza harufu mbaya mwilini.

Mwezi Januari 2013, wataalamu wa vinasaba vya ngozi katika Chuo Kikuu cha Bristol, Ian Day na Dkt. Santiago Rodriguez, walishirikiana kufanya utafiti kuhusu viondoa harufu ambapo walifanya utafiti kwa wanawake 6,495. Wataalamu hao waligundua kuwa asilimia 2 ya washiriki (wanawake 117) walikutwa na kinasaba cha ABCC11. Kati ya wanawake hao 117, asilimia 78 walikuwa wanaendelea kutumia deodorant ingawa hata hawakuwa wakilazimika kufanya hivyo kama wenzao.

Ingawa utafiti huu wa Day na Rodriguez haukuhusisha wanaume, Day aliiambia LiveScience kuwa anadhani matokeo ya utafiti huo yanaweza kutumika kwa wanaume pia na kutoa matokeo yanayofanana. Pia, katika mahojiano aliyofanyiwa, alikadiria kuwa asilimia mbili ya Wazungu na karibia watu wote wa Mashariki mwa Bara la Asia na Wakorea wana vinasaba vya aina hii.

“Matokeo haya yanaweza kumuongoza mtu kutumia Elimu ya vinasaba vya mwili wake kutambua na kuchagua aina ya vipodozi na bidhaa za usafi wa mwili wake,” alisema Rodriguez alipokuwa anazungumzia umuhimu wa matokeo ya utafiti huo. “Kipimo cha kawaida cha vinasaba kinaweza kukuongezea hali ya kujijua zaidi na kukuepushia gharama zinazotokana na matumizi yasiyo na ulazima wowote na pia kukuepusha na matumizi ya kemikali zilizopo kwenye bidhaa zinazozuia harufu.”

Kwa wenzetu ambao huwa wanatokwa jasho sana likiambatana na harufu mwilini, jaribu kufuata ushauri huu:


  • Jaribu kutumia kitoa harufu (deodorant) aina ya ‘Rx-strength,’ ambayo inawasaidia sana kwa watu wanaotokwa jasho jingi kwenye makwapa, viganja vya mikono au kwenye nyayo za miguu.
  • Hakikisha unapaka kitoa harufu chako nyakati za usiku, kwakuwa itakusaidia kuviweka vizuri zaidi vinyweleo vinavyotoa jasho kwa muda huo kuliko unapoipaka au kujipulizia asubuhi.
  • Jaribu pia kutumia sindano aina ya ‘Botox’ ambazo zinasaidia kuzuia mtiririko wa taarifa zinazoruhusu mwili kutoka jasho kutoka kwenye ubongo sizifike sehemu iliyochomwa sindano.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad