KIMENUKA...CUF ya Lipumba Yatangaza Vita Kwa Chadema.....


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Bara anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Magdalena Sakaya, amejibu mapigo baada ya mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kutangaza jana ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’. Kubenea amedai kuwa oparesheni hiyo inalenga kumuondoa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Akijibu mpango huo uliotangazwa na Chadema inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Sakaya ambaye ni kambi ya Profesa Lipumba alisema kuwa anawasikitikia Chadema kwa kuingilia mgogoro usiowahusu.

Sakaya ameongeza kuwa Mpango huo wa Chadema hautafanikiwa kamwe na kwamba wanachokifanya ni Kuingilia mambo yasiyowahusu.

Katika hatua nyingine, Kubenea alipozungumzia majibu ya Sakaya amedai kuwa CUF ni sehemu ya Ukawa, hivyo inapoonekana inataka kudhoofishwa ina maana kuwa Ukawa itadhoofika pia, hivyo hawako tayari kuliona hilo.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna Nini Tanzania. Inaficha nini ukweli wa kisiasa. Watu dhidi ya Msajili? ni nini hii? Vipi sheria zinazochezewa na nchi hii kuleta mivurugo isiyo na miguu. Mtu kajiuzuru. Serikali inamsajili tena kwa kulazimisha ambapo watu walimkataa. Na huyu baba hapo juu yupo na utumbo kila gazeti nikimaanisha Leonidas Kabugumila. Huyu ni CCM . kila kitu kinachofanywa na CCM kwake ni halali. Hayupo peke yake, kuna Watanzania wengi kwenye changamoto za fikra hawana kabisa. Ni hatari kama Taifa letu limejaa na watu wa namna hii. Ni mzigo mkubwa na ni pingamizi kubwa kimaendeleo na kielimu. Watu kama hawa hata ukiwapeleka shule hawatafungua kitabu wakasome na kujielimisha. Hata ukifungua kitabu ukamwekea mbele yake atadadisi kwa nini asome ameshajua jibu. Majuha kama hawa ni wengi mno. Wavivu wa kufikiri, waoga wa uhuru, na ni janga kuu kwa Taifa letu. Utamwkuta haungi mkono kumsomesha binti hata baada ya kujifungua sababu tu, Raisi kasema. Hawatumii alikili ni viraza vukubwa. No hope kwa watu kama hawa. Mambo ya kulazimisha inabidi yakemewe na kila mtanzania sababu yanahatarisha amani nchini. Wengi hawa wanasiasa ni pesa zinawasumbua sababu wakitoka kwenye siasa hawajui namna ya kujiajili wenyewe. Hawana uwezo. Siasa ndiyo chakula chao. Na usomi wote walionao wanko radhi kuwavuruga wananchi kwa maslahi binafsi.Kama Lipumba kwa nini asifundishe mambo ya uchumi. Akatumia elimu na kuwakimboa watu kwa mafunzo ambayo wengi Tanzania wangefaidika. Amezoea pesa rahisi tu Siasa.Hata akijua analigawa Taifa. Nyinyi wasomi mnaharibu Taifa hili.Inabidi muwekwe ndani kwa kuhatarisha usalama wa nchi hii. Nashangaa CCM dar inamwachia achafue amani hata ndani hawamweki hata. Kuna nini wakuu wa mkoa Dar na Wilaya. Mnamwona Lipumba anaharisha usalama, watu wanapigana lkini hamumchukulii hatua badala yake polisi inamlinda. Hii mpya. ingekuwa mtu wa chadema angesweka ndani hata bila kosa lolote. Ndo sheria potofu hizi. Za upendeleo na uonevu kwa wengine.Ndo CCM yetu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama yeye ni CCM we ni ukawa.....hakuna la maana unaloongea aisee...we utakuwa umetumwa naona...

      Delete
  2. Taratibu za kujiuzulu Lipumba zilifuatwa? halafu iweje CHADEMA wacheze ngoma ya maalim Seif kuna nini? unaweza kutupatia majibu ya haya?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad