KIMENUKA..Wafanyakazi Flyover Tazara Wagoma


WAFANYAKAZI wa kampuni ya LABA Construction Ltd ambao ni vibarua wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction company Ltd inayojenga barabara ya juu (Flyover) ya Tazara wamegoma wakishinikiza kuongezwa maslahi yao pamoja na kuitaka kampuni ya Laba kuondoka.

Wafanyakazi hao walianza mgomo kuanzia siku ya jana ambapo wanaitaka kampu ni ya Laba ambayo wanadia inafanya kazi ya udalali kuondoka kwa kuwa ndio inawanyonya kwani kampuni ya Sumitomo imekuwa ikilipa Sh 37,000 kwa fundi na kibarua Sh 25,000 lakini kampuni hiyo imekuwa ikilipa Sh 14,000 kwa fundi na Sh 10,000 kwa kibarua.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa wafanyakazi hao Jackson Mselemu amesema, wanachodai ni kutaka kuongezewa maslahi n akwamba wanataka yalipwe moja kwa moja bila kuwepo mtu wa kati ambayo ni kampuni ya LABA.

"Hii kampuni ya LABA ndio inatudhulumu , tunakatwa hela za PPF lakini tumeenda kuuliza tunaambiwa hakuna hela iliyowahi kupelekwa kuele, kwa hiyo sisi tunaomba mtusaidie, lakini pia hatutaki fedha zetu zilipwe kupitia Tigo Pesa, tulipwe kwa njia ya benki," amesema Mselemu.

Naye Hussein Bakari amesema, kwenye mfuko wa PPF wameambiwa kampuni ya LABA haitambuliki hivyo ni vyema wakarudi kwa mwajiri wao ili wapate ufafanuzi mzuri, lakini hakuna pesa  yoyote iliyopelekwa kwa ajili yao.

Mashaka Nyerere amesema, hawajagomea kazi bali wanachokigomea ni maslahi kwa kuwa malipo wanayoyapata hayaendani n akazi wanazofanya. Alisema kazi wanazofanya ni ngumu na zinafanywa katika maeneo ya hatari, lakini maslahi wanayopokea ni mabovu.

"Sisi tuko tayari kufanya kazi lakni tunataka hii kampuni ya udalali ya LABA iondoke tuko tayari kufanya kazi tukalipwa hata Shilingi elfu kumi na Mjapani, kwasababu tunajua tutambana wapi kuliko huyu mswahili," amesema Nyerere.

Kwa mujibu wa mkataba baina ya kampuni ya LABA na mfanyakazi unaonesha malipo ya kazi kwa saa ni Sh 1,250, kwa siku Sh 10,000, malipo baada ya muda wa kazi kuisha Sh 1,875 kwa saa na siku ya jumapili na sikukuu Sh 2,500 kwa saa huku ikiwa na sehemu ya kujaza namba ya simu iliyosajiliwa na Tigo Pesa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad