Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya jaribio la kombora lake la pili la masafa marefu ICBM, huku ikitoa onyo kali kwa Marekani kuwa inauwezo wa kushambulia eneo lolote lililopo nchini humo.
Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amesema kuwa jaribio hilo limebaini kuwa Marekani yote ipo katika rada ya Korea Kakazini na sasa inaweza kushambuliwa wakati wowote kwa makombora hayo.
Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa jaribio hilo ni la kijinga na ni kitendo cha kichokozi na cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini, ambapo ameongeza kuwa hali kama hiyo isipodhibitiwa inaweza kusababisha athari kubwa kwa jamii.
Kombora hilo lilionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko lile la kwanza.
Kombora hilo lililoanguka karibu na ufuo wa Japan limeshutumiwa kimataifa huku Rais Donat Trump akisema jaribio hilo lilifanywa kiholela na ni hatari.
Kombora hilo lilionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko lile lililojaribiwa mapema mwezi huu kwa kuwa lilikuwa angani kwa zaidi ya dakika 47, kulingana na taarifa zilizotolewa na Pyongyang na ambapo lilienda kwa mwendo wa kilomita 1,000. Lilidondoka karibu na Ufuo wa Japan.
Vikosi vya kijeshi vya Marekani na Korea Kusini vilivanya zoezi la kijeshi kwa pamoja ambapo makombora kadhaa yalilipuliwa na wizara ya ulinzi kutangaza kuwa silaha maalumu zitawekwa nchini humo.
Muda mfupi baada ya jaribio hilo, Korea Kusini, Japan na Maafisa wa Marekani waliripoti data kuhusu eneo na umbali, pamoja na muda uliochukuliwa na kombora hilo.
==>Ijapokuwa tathmini kamili haijakamilishwa, vitu kadhaa vilibainika.
Kwanza, data iliyopo inaonyesha kuwa kombora hilo lina uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 10,400.
Kombora hilo linaweza kurushwa na kufika mji wa New York.
Pili Marekani iliripoti kwamba Korea Kaskazini ilirusha kombora hilo kutoka Mupyong -ni Korea Kaskazini.
Eneo hilo lilikuwa tofauti ikilinganishwa na taarifa za awali ambazo zilifanikisha jaribio yaliotabiri kurushwa kwa kombora la Kusong.
Hata hivyo, China imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pande zote zinazoshutumiana kuvumiliana na kutoendelea na majaribio hayo kwani yanaweza kusababisha madhara makubwa na kuhatarisha usalama wa eneo husika.