Kukamatwa Kwa Tundu Lissu Hakuwezi Kumwacha Mtu Salama...Wanasheria Afrika Mashariki Waliamsha Dude

Wakati wenzao wakisema makosa manne ndiyo yanayoweza kumlazimu mtuhumiwa kupimwa mkojo, Jumuiya ya Afrika Mashariki imesema inafuatilia sakata la mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi.

Lissu, ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alikamatwa Alhamisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akisubiri kwenda Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano wa jumuiya hiyo.

Wanasheria wa Lissu wamesema waliambiwa na polisi kuwa amekamatwa kwa tuhuma za uchochezi, lakini alitakiwa kutoa kipimo cha mkojo, jambo ambalo limezua maswali.

“Tutafanya mipango ya kufuatilia kesi ya Wakili Tundu pamoja na mchakato mwingine wowote wa mahakama ambao umeshafikishwa mahakamani au unaweza kufikishwa mahakamani, kwa niaba yake kuthibitisha haki za Mtanzania kama zilivyoelezwa na sheria ya kimataifa,” inasema taarifa ya Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) iliyosainiwa na rais wake, Richard Mugisha.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa EALS inachukulia kukamatwa kwa Lissu kama ishara nyingine ya kuendelea kuzorota kwa uhusiano baina ya Serikali na TLS, hali iliyoanza wakati wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

“Ni kitu kilicho wazi kuwa uhusiano huo umekuwa ukiharibika tangu kipindi cha kuelekea na baada ya matokeo ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa TLS ambao Wakili Lissu alichaguliwa na wanasheria wenzake kuongoza TLS kwa mwaka mmoja,” anasema Mugisha.

Wakati EALS ikitoa msimamo huo, wanasheria nchini bado wanahoji sababu za Lissu kuchukuliwa kipimo cha mkojo wakati akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi.

Kwa mujibu wa wanasheria hao, makosa yanayoweza kusababisha mtuhumiwa achukuliwe kipimo hicho ni ya usalama barabarani, matumizi ya dawa za kulevya, ubakaji na mashauri ya ndoa na watoto ambayo hulazimu mkemia kupima sampuli hizo.

Lakini Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema uchunguzi wa polisi hauna mipaka na kwamba jeshi hilo halifanyi kazi kwa mihemko ya watu, bali kwa kuzingatia weledi.

Alisema kitendo cha watu kuhoji suala la Lissu kupimwa mkojo ni kuingilia uchunguzi. Alisema uchunguzi ni suala pana, hivyo kuwataka wasubiri mtuhumiwa huyo atakapofikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yake.

“Kwenye suala la ku-suspect (kutuhumu), polisi anaweza ku-suspect anything (kitu chochote) kutoka kwa mtu yeyote. Siwezi kuelezea mikakati na mbinu za kiuchunguzi, lakini mtambue kwamba uchunguzi is too general (ni mpana), unaweza kuchunguzwa kwa mambo mengi,” alisema Mwakalukwa.


Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. R.muigisha na J.Banda.. kwa taarifa yenu na wenzenu wenye mwelekeo kama wenu. Ni ukimbusho na taarifa kwenu kwamba. kuongilia kazi ambazo hamna majukumu nazo ni ukosefu wa muelekeo na ubabaishaji ambao hatuutegemei. Tuachieni tufanye kazi zetu amnazo ni majukumu yetu. ikiwa mtahotajika tutakupeni taarifa na mwaliko rasmi. pondi na hapo itakapo tokea. Na hili si suala la mitandaoni. mnaweza kuchukulia hii kama.....nyo..msiendelee kuleta yasiyo kuwepo na kwa wakati ambaao si muwafaka kwa hili. Kisu tunae na upelelezi unaendelea mpaka hapo tutakaporidhika na kuamua kitakacho endelea. Tulieni.

    ReplyDelete
  2. Ndugu mwandishi..!!! ulikuwa na utashi gani katika kuandika hili. Kichwa na taarifa haziendani. nakushauri urudi kupata Refresher course kama inahitajika toka kwa muajiri wako..!!! POLE NDUGU YANGU. KUMBUKA TAIFA LINAHITAJI WELEDI WAKO WAKATI WOTE

    ReplyDelete
  3. Kwa kukusaidia kutokana na jinsi ulivyo. Kwa ufupi wewe huhitaji kuijua sheria vilivyo. Ila nakwambia sheria ni mfumo wa maisha ambao Jamii inakubali na kuridhika kuwa atakae endea kinyume basi amevunja sheria. Hapo ntakuwa nimekusaidia kuijua sheria. au ukitaka nikurudishe darasani sidhani kama utaweza kunielewa na mimi nikutendee haki vilivyo. Unaweza ukapitia maadhi ya Mada alizo andiaka Dean wetu wa Fuculty of Law Prof Kadudi. Mdogo wa Kukaya. Mzelelo alimsomi Du!! Na Gwegwe Ulimzinzi Du!! Uwalamsaje Kukaya...( Nakuombe mungu ujielewe na uelewe)

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad