Madhara Yatokanayo na Kuvaa Sidiria Ndogo 'Kubusti' ili Kunyanyua Maziwa

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wanawake kunyanyua maziwa yao, ambapo watu wengi hufahamu kama ‘kubusti’, bila ya wao kujua kuwa jambo hilo lina madhara katika afya yao.

Ili kuweza kubusti, wanawake hulazimika kuvaa sidiria ambazo ni ndogo kuliko ukubwa wa maziwa yao na hivyo kuyabana. Baadhi ya wanawake hununua sidiria hizi bila kujua ukubwa halisi wa maziwa yao na hivyo kujikuta wakibusti bila kupenda wakati wengine hudhamiria kabisa kununua sidiria hizo.

Kufuatia utafiti uliofanywa na timu ya wataalamu Lingerie Curvy Kate kutoka nchini Uingereza ulionyesha kuwa wanawake asilimia 95 huvaa sidiria zisizo na ukubwa sawa na matiti yao jambo linaloweza kusababisha uharibifu wa tishu mihimu katika matiti (kifua).

Timu hiyo ilitumia aina mbili za sidiria. Ya kwanza ni ile iliyokuwa ndogo kuliko matiti na nyingine ilikuwa sawa na matiti na kumvalisha mwanamke na kisha kumtaka atembee ili kuweza kugundua tofauti iliyopo.

Kupitia utafiti huo waliweza kugundua kuwa , madhara ya kiafya yanaweza kumpata mwanamke ambaye anavaa sidiria isiyoendana na ukubwa wa maziwa yake.

Mtaalamu mwingine, Chantelle Crabb alisema, uvaaji wa sidiria ambayo haiendani na ukubwa wa maziwa ya mwanamke kunaweza kusababisha maumivu ya matiti, aibu na uharibifu wa matiti. Lakini alifafanua zaidi kwamba, uvaaji vibaya wa sidiria unaweza kupelekea matiti ya mwanamke kulegea/kulala.

Mbali na hayo, madhara mengine ni pamoja na maumivu ya mgogo kwani mwenye maziwa makuba akivaa sidiria ndogo hulazimika kuinama anapopita katika eneo lenye mwinuko.

Maumivu ya bega ni madhara mengine yatokanayo na uvaaji wa sidiria ndogo kutokana na kamba za sidiria kuyabana mabega yako kwa nguvu.

Kuhusu kupata saratani ya matiti/titi, Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Cyrill Massawe alisema kuwa,  wanawake wanapaswa kuvaa sidiria zinazoendana nao ili wawe huru, huku akisema hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuvaa sidiria ndogo na saratani ya matiti.

Chanzo: Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad