Amesema kuwa, Maalim Seif kwa sasa hajielewi kwani CUF inaendeshwa kwa kufuata misingi ya Katiba ya chama hicho si kama Maalim anavyofikiria kukiongoza chama hicho cha upinzani.
Ameyasema hayo mara baada ya kikao kinachodaiwa kuwa cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho kilichofanyika mjini Unguja na kuwafukuza wanachama saba wa chama hicho akiwemo Sakaya.
“Naona sasa uwezo wa kufikiri wa Maalim Seif unazidi kupungua, sijui sasa anafukuza watu kwa mara ya ngapi, hajui anachokifanya kwa sasa, kila siku amekuwa akikurupuka tu katika kutoa maamuzi,”amesema Sakaya.
Hata hivyo, amesema kuwa CUF ni chama kimoja chenye Mwenyekiti na Katibu mmoja huku manaibu katibu wakuu wakiwa wawili na kila maamuzi yanafanyika kwa kufuata Katiba ya chama hicho.