Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo leo, imeelezwa kuwa sababu ya kukata maji ni kuzima mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu ili kukamilisha mfumo wa umeme kwa mtambo mpya.
Dawasco imesema mtambo huo wa Ruvu Juu upo Mlandizi, Pwani na kuwataka wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi hicho.
Taarifa hiyo iliyataja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu na Picha ya Ndege.
Mengine ni Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba njia panda shule ya Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Kimara, Ubungo na baadhi ya maeneo ya Tabata.