Taarifa ya Vikosi maalum vya kulinda amani vya umoja wa Mataifa(MONUSCO) ilieleza kuwa makaburi mengine 38 ya pamoja yaligundulika katika mkoa wa Kasai.
Idadi hii inapelekea kufikia jumla ya makaburi ya pamoja 80 ambayo yamegunduliwa tangu mwaka uanze.
Makaburi haya 38 yaligunduliwa katika maeneo ya Diboko na Sumbula katika ukanda wa Kamonia.
Eneo la Kasai ni makao makuu ya kundi la kijeshi la Kamuina Nsapu. Mgogoro na serikali uliongezeka mnamo mwaka 2016 baada ya vikosi vya serikali kumuua kiongozi wa kundi hilo.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwezi Aprili, zaidi ya watu 400 wamefariki tangu mapigano kati ya majeshi ya serikali na wanamgambo hao yapambe moto.