Matokeo Kidato cha Sita : Wasichana Waongoza kwa Kufaulu


Matokeo ya kidato cha sita nchini  yalitolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo  kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).


Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.


Kwa upande wa watahiniwa wavulana,  waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya  46,385.


 Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.


 “Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11  umepanda  kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;


 “Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”


 Ufaulu wa masomo

Kadhalika taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti kubwa ukilinganisha na mwaka jana.


Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad