Mawakili wa Lissu Wazuiwa Kumuona


Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema mpaka sasa hajaruhusiwa kumuona mteja wake licha ya kufika Polisi Makao Makuu tangu asubuhi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Julai 21, Karume aliyekuwa na wakili mwingine wa Chadema, Peter Kibatala amesema wameambiwa Lissu hatapelekwa mahakamani kwa sasa kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

“Tupo hapa tangu asubuhi, tunaambiwa hatuwezi kumuona kwa sasa, lakini jambo la kushangaza ni kuwa tunaambiwa hatapelekwa mahakamani kwa kuwa uchunguzi haujakamilika ingawa kosa bado halieleweki,” amesema.

Amesema polisi wamewaambia mawakili wa Lissu kuwa hata dhamana kwa leo haitawezekana kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ei ei naliya, nalilia nchi yangu, nchi yangu Tanzania.

    Nchi yetu ya amani, nchi yetu tskatifu, nchi yetu ya mababu.

    Ei eli nalia. Nalilia nchi yangu.nchi yangu ya amani.

    ReplyDelete
  2. Tunakuombeni na kuwapa taarifa kwamba upelelezi wake utachukua si chini ya siku 180. sababu yake ni kwamba tunaangalia uhusiano wake na baadhi ya washirika waliojitokeza hivi karibu huko uaghaibuni. kwa hiyo tumeshaanda timu ambazo zitaanza Safari za masafa marwfu . na kama mnavyo jua kuna maandalizi ya usafari wa nchi za nje ikiwemo Upatikanaji wa Visa za nchi husika mbali mbali. Zoezi tumeshalianza tunaomba uvumilivu na ustahamilivu wenu. Yupo kwetu katika mikono ya usalama na salama. Tutawaataarifu ikiwa kunahitajika. Tanzania yetu ni ya Amani na Salama. na kila mtaka vunja amani to Umguja mpaka kigoma Tutamshughulikia ipasavyo. Kwa hiyo pumzikeni na mtulie TULI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad