MCHEZAJI Elias Maguli Alivyoulizwa Swali Kwa Kingereza na Mtangazaji na Kujibu Kiswahili Baada ya Kuibuka Mchezaji Bora Mechi ya Jana

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wameichapa timu ya Taifa ya Afrika kusini kwa bao 1-0 ambao ndio wenyeji wa michuano ya kombe la Cosafa inayoendelea huko nchini Afrika Kusini.


Bao la dakika ya 18 la mshambuliaji Elias Maguli lilitosha kuipeleka Stars katika nusu fainali ya michuano hiyo katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Royal Bafokeng, Rusternburg.

“Ahsante sana namshukuru mwenyezimungu kwa kutuaajilia kuweza kupataushindi katika mchezo huu. Ulikuwa mchezo muumuu sana ila tunamshukuru mwenyezimungu kwa kutujaalia kuweza kutoka na us hindi na washukuru mashabiki waliojitokeza na kuweza kutushangilia na kutupatia nguvu”. Alisema Elius Maguli ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.


Tanzania sasa itamenyana na Zambia siku ya Jumatano katika mchezo wa nusu fainali, wakati Afrika Kusini wanaangukia kwenye michuano ya Plate, inayoshirikisha timu zilizotolewa hatua ya robo fainali.

Katika mchezo wa pili wa michuano hiyo Zimbabwe waliwachapa Swaziland kwa jumla ya mabao 2-1.

TAZAMA VIDEO HAPA:

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad