Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika mpaka sasa amekamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Shenzhen nchini akitokea Hong Kong na simu aina ya iPhone 102 akiwa amezifunga kiunoni tayari kwa kuziingiza nchini humo kiholela.
Mwanamke huyo aliyejifunga simu hizo kiunoni kwa kutumia tepu huku akiwa amevalia nguo nzito nzito alishitukiwa na wahudumu wa uwanja huo wa ndege baada ya kubaini muonekano wake kutokuendana na viungo vingine kama mikono na miguu.
“Tulimuona akiwa na wasiwasi na aliyevaa nguo nzito nzito ilehali kwa sasa ni kipindi cha joto ndipo tukapatwa na mashaka nae tukaanza kumkagua zaidi”,amesema mmoja wa Wahudumu wa Uwanja wa ndege wa Shenzhen nchini China kwenye mahojiano yake na mtandao wa News in China.
Wakaguzi hao wamesema walimkuta na simu na saa za mikononi ambapo kwa ujumla vilikuwa na uzito wa Kilogramu 19 .
Mharifu akiwa amebeba mzigo wake wa iPhone
Hata hivyo tukio hilo sio la kwanza kutokea nchini China kwani mwaka 2015 mwanamme mmoja walikamatwa na simu aina ya iPhone 146 uwanjani hapo wakijaribu kuingiza simu hizo kiholela nchini China.
Watu wengi wanafanya biashara hiyo kutokana na bei ya simu aina ya iPhone kuuzwa bei kubwa ukilinganisha na bei inayouzwa simu hizo, Hong Kong.
Serikali ya China ilitangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa zote za Kampuni ya Apple INC ili kuchochea mauzo ya bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.
Mrembo Anaswa Airport na iPhone 102 Kiunoni Akiziingiza China (+Picha)
0
July 24, 2017
Tags