Katika mahojiano maalum na Global TV Online, Julius ambaye anajulikana zaidi kama Mr. Shinda Nyumba, kufuatia ushiriki wake kwenye kampeni ya uhamasishaji wa shindano hilo kwa wasomaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani na Championi, alisema kiasili ni mkazi wa Mwanza, akiwa mtoto wa pili kati ya saba waliozaliwa kwenye familia yao ambapo kwa sasa ana miaka 21.
Julius alianza kujiona tofauti akiwa Darasa la Sita, kwani alianza kujigonga mara kwa mara mlangoni huku watu wakiwemo ndugu zake wakianza kushangazwa na aina ya ukuaji wake na nyakati zingine kugeuka kivutio na mshangao kwa wanafunzi wenzake na watu wengi waliokutana naye.
“Nimeanza kuonekana mara kwa mara kwa siku za hivi karibuni tu, nilikuwa najificha ndani muda mwingi nikiogopwa kushangaliwa na watu, nakumbuka kuna siku nilikuwa naelekea nyumbani majira ya usiku nikakutana na jamaa, aliponiona alianza kukimbia huku akipiga mayowe, nikajitahidi kumuelewesha kuwa mimi ni binadamu wa kawaida, lakini bado akazidi kukimbia, huwa najisikia vibaya ni kama mateso kwangu.
“Lakini pia kwa upande wa faida ni kwamba nilisomeshwa bure na mzee mmoja ambaye ni Meja wa Jeshi, Idd Kipingu baada ya kuvutiwa na urefu wangu hivyo akanisajiri kwenye timu ya basketball, malengo yangu ni kwenda nchini Marekani kutimiza ndoto yangu ya kucheza kikapu, Hashim Thabeet huwa ananifariji sana, tunafahamiana,” alisema Julius au Mr. Shinda Nyumba. VIDEO: