Mwanamziki Diamond Video Tatu Ndani ya Mwezi Mmoja za Nini zote Hizo?

Kwanza kabisa nakupongeza sana kaka kwa kazi nzuri sana, pia mimi nishabiki wako kwa kiwango cha lami.

Sasa najiuliza kwanini umeachia video tatu kwa wakati mmoja( Fire, I miss you na Eneka) zote hizo za nini bado hujiamini? Kumbuka wewe ni msanii mkubwa sana hapa Tanzania na Africa unakimbia unaenda wapi na hizo video yaani wakati mimi natafakari single yako ya fire jinsi ilivyo nzuri mara naona single ya I miss you sijakaa sawa naona Eneka.

Mwisho kabisa naomba uachane na mtindo huu unatuchanganya mashabiki wako kaka toa single moja tupe mda wa kuenjoy na single moja kwa mda mrefu kama ulivyofanya kwa single ya Merry you.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna kiumbe wa ajabu kama binadamu yeye ni kiumbe wa ku-complain tu all the time likiwaka jua utamsikia oh hili jua nishai sana joto mtindo mmoja haya ikianza kunyesha mvua utamsikia binadamu huyo huyo ana-complain kuwa ah hizi mvua za mshindo bana nishai kweli kweli sasa ndiyo hayo hayo ya huyo mr complainer wa habari hizo hapo juu kuhusu video 3 mfululizo za mbongo flava akikaa kimya utasikia ah ameishiwa hana mpango eh katoa video 3 mfululizo oh kwanini amefanya hivyo angengojea kwanza duh!in fact bindamu ni kiumbe dhaifu sana sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad