Mwimbaji Diamond Platnumz na Mabomu yake Kama ya Korea Kaskazini...


UNAPOTAKA KUINGIA KWENYE VITA LAZIMA UHAKIKISHE UNA SILAHA ZA KUTOSHA.

Wakati dunia nzima inaangalia mzozo baina ya Korea Kaskazini na Marekani utamu unakuja kwa Rais wa Korea kaskazini ambaye yeye hana maneno sana zaidi ya kuendelea kufanya majaribio ya silaha zake.

Katika muziki Tanzania mfano wa rais wa Korea kaskazini Kim ni @diamondplatnumz .Wakati mashabiki wanalalamika kuwa jamaa anachelewa kutoa ngoma alisema anataka ku push vijana wake kwanza ndio naye aachie sasa nahisi amepania kukata kiu ya mashabiki wake.

@diamondplatnumz ndani ya muda mchache ameachia makombora ya masafa marefu na mafupi yani I MISS YOU,FIRE na ENEKA ila kabla ya mashabiki hawajakaa vizuri wanapata taarifa kutoka kwa @patorankingfire kuwa mwezi ujao wanaachia bomu la masafa marefu majini ndani yake akiwemo tena @diamondplatnumz .

Kitu ambacho kinamfanya @diamondplatnumz kuwa kama Rais wa Korea kaskazini ni kutosikiliza criticism za maadui wake na kuendelea kuachia silaha zake ila watu wasichojua kila silaha ina target zake.
Nilisema ngoma ya FIRE target yake ilikuwa kumuweka @tiwasavage ambaye ndani yake kuna #rocknation chini ya #JAYZ mpaka hapo lazima Fire imepita machoni mwa #Jigga.
Lakini #ENEKA watu wanasema ni sample beat ya #FALL kutoka kwa @davidoofficial lakini ukweli hiyo inaweza kuwa sababu inayofanya ngoma hii ina heat kwa kasi sana maana wanavyozidi kulinganisha ndio wanaipa rotation.

@diamondplatnumz ni mfanya biashara wa muziki kwa mana hiyo akiona mtu anauza matikikiti na anauza sana naye anapeleka matikikiti pale pale ili wagombanie wateja mwisho wa siku wakitoka pale kila mtu kauza.

Leo jiulize #FALL ya @davidoofficial inavyokimbiza halafu ndani yake imeletewa pacha wake #ENEKA unategemea nini hapo lazima zote ziende kwa kasi.

@diamondplatnumz ameonesha nia ya kupambana na @wizkidayo @davidoofficial na kina @teknoofficial na njia nzuri ya kupambana nao ni kupeleka bidhaa kama zao nazo ndio hizo #eneka na #fire.

Music is business and business is all about creativity ndio mana diamond anafanikiwa mana anafanya biashara ya muziki.

RAHA YA VITA UWE NA HAZINA YA SILAHA KWENYE GHALA.
.
By @Abby1_thebest
@abby1_thebest
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wacheni uchochezi diamond kazidi nini alisimama na kuimba direct no alijifunza na akafundishwa na hao hao anaowaita maadui so calm down mungwana lake rohoni muone King he is not type of bla bla anaonyesha action to so kuwa kiakili na sio ushindani you will never reach anywhere

    ReplyDelete
    Replies
    1. aisee mbona hueleweki ulichokiandika??? au ndo wale wale wanaoandika upupu?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad