Nahisi Mke Wangu Anatembea na Binamu yake....


Mimi ni mwanaume wa Dar kabisa nina kifriji cha bia za ofa na kitimoto na kazi yangu huwa ni upambe kwa matajiri na watoto wa mjini japo nina kiofisi cha kuzuga cha insurance broker na clearing and forwarding kama ilivyo ada yetu wanaume wa Dar.

Sasa balaa linalonikabili ni hivi juzi wife aliniomba aje mtoto wa shangazi yake akae kwangu kwa kuwa alipata fursa ya kujifunza kazi ya ufundi magari gereji ya karibu na nyumbani kwangu. Bila hiyana nikamkubalia, sasa balaa tulipoenda kumpokea Ubungo kushuka kijana bonge la handsome afu mwili wa mazoezi.

Kimsingi wamezoeana sana na wife. Akiamka asubuhi mimi naandaliwa chai sausage na yai yeye anapasha kiporo cha ugali anashushia na mchicha anaoulima bustani hapa kwangu. Baada ya hapo anaenda jogging akirudi ndo anaelekea gereji mayaweee nafwa

Gereji wanatoka saa 8, kuna siku nikarudi ghafla mchana nikakuta amekaa na boxer na singlet miguu bonge la gimbi kifua kimejaa minywele afu anapiga pasi nguo za wife mwee ndifwaaa mwiyenu

Kinachoniudhi anajifanya ana heshima sana kwangu mara anipokee mizigo mara amsindikize wife sokoni aghhhggaaaaa come on shittt.

Sasa juzi kati walitoka na wife kumpeleka sokoni sijui kilinikumba nini nikaingia kupekua chumba chake nikakuta kitenge cha wife kitandani kilichopigwa pasi nikajifariji itakuwa ni hii tabia ya kumpigia pasii cheki kwenye droo nikakuta mafuta ya 'KY Gel' ila hayajatumika kabisa.

Kumuuliza wife naona nitapoteza ushahidi au nitaharibu uchunguzi basi nimekuwa kila wakitoka nakagua yale mafuta, ni wiki sasa hayajafunguliwa.

Jamani watemi nitumie gia gani kumtimua huyu maana nimejikuta narudi saa nane kumhofia jamaa.
.
.
NAOMBENI USHAURI TAFADHALI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad