NAMSHAURI Malinzi Ajiuzulu Urais wa TFF ili Amalizane na Jamhuri

Nasema mwanzo mwanzoni kuwa mimi ni Mwanasheria na Wakili Msomi. Najua kuwa kutuhumiwa na kushtakiwa si kukutwa na hatia. Kila mshtakiwa si mwenye hatia hadi mahakama itamke hivyo. Mambo hayo,kama moja ya haki za msingi za binaadamu,nayajua na kuyaheshimu.

Rais wa TFF,Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wake Mwesigwa wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya jinai mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha. Kabla ya hapo,Malinzi alikuwa moja ya waliochukua fomu za kugombea tena Urais wa TFF.

Ili kupunguza mzigo wa mambo na kukubali yaliyompata kimaisha,namshauri Jamal Malinzi ajiuzulu Urais wa TFF ili apate nafasi ya kumalizana na Jamhuri kwenye kesi yake ya jinai. Kuendelea kuwa Rais wa TFF akiwa mshtakiwa kunaweza kutafsirika kama kung'ang'ania kichaka chake cha 'kupiga dili'.

Kujiuzulu,pamoja na kupunguza mzigo,kutamfanya Malinzi awajibike ipasavyo kwa yaliyompata na kukubali kilichomkumba kimaisha. Hakuna haja ya Mshtakiwa kuendelea kuwa Rais wa TFF au hata kujadiliwa kama mgombea mtarajiwa wa Urais wa TFF. Apambane kwanza na jinai yake.Kujiuzulu,wakati mwingine,huilinda punje ya heshima iliyobaki!

By Petro E. Mselewa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad