“Nikiondoka Hakuna Atakayekuwa Kama Mimi” – Kauli 7 za Rais JPM

Rais Magufuli leo July 25, 2017 ameendelea na ziara yake ambapo alikuwa katika Mkoa wa Singida alikozindua Barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa km 89.3 ambapo mbali na kufanya uzinduzi huo alipata nafasi ya kuhutubia wananchi.

Nimekusogezea mambo 7 makubwa kati ya mengi aliyozungumza kwenye hotuba yake.

'Pengine nikiondoka mimi hakuna atakayekuwa kama mimi, nasafisha njia ya Rais atakayekuja baada ya mimi' - Rais @MagufuliJP

'Ni lazima niyatapike yote haya, nikikaa nayo nitapata presha bure, ila wale walioyafanya wakumbuke na madhambi yao' - Rais @MagufuliJP

'Suala la ubinafsishaji mimi silipendi kabisa, siwezi nikawalaumu waliofanya hivyo lakini pia siwezi nikaacha kusema' - Rais @MagufuliJP

'Nataka Tanzania hii iwe kama Ulaya na tutafika tu, lakini ili tufike huko ni lazima tutabanana kweli kweli'- Rais @MagufuliJP

'Wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza tu kuanza kubomoa taratibu nyumba zao'- Rais @MagufuliJP

'Niliporudishwa wizara ya ujenzi nilimfukuza Chief Executive Officer ndani ya siku 3 kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha' - @MagufuliJP

Wengine mmewachagua lakini wanaongelea ya mambo Dar es salaam tu kosea kuoa unaweza kutoa talaka lakini usikosee kuchagua - Rais @MagufuliJP

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh!Kauli hiyo ni ya kibabe na kutishana

    ReplyDelete
    Replies
    1. hujielewi na wala hutamwelewa Rais wetu

      Delete
  2. Ni kweli, kwa bara hili. Hiliiiiii!!!!!!! Bara jeusiiiiii hataaaa hakuna baba Magu, Watu weusi na roho zao nyeusiiii Pia.

    ReplyDelete
  3. Alafu ni uzandkiki na upotoshaji makubwa wa habari au kauli za muheshimiwa raisi. Muheshimiwa raisi hakusema hakuna atakae kuwa kama yeye. Kuweka taarifa sahihi alichokisema muheshimiwa Magufuli ni kwamba inawezekna kabisa kiongozi atakaekuja baada ya yeye akashindwa kutenda anayoyayenda yeye hivi sasa. Chukua neno "inawezekna " katika kauli yake kwa maana yakwamba inawezekna hata akapatikana kiongozi mazuri zaidi ya yeye, tunaomba wahusika wa habari muache kupindua maneno kwani sio vizuri hata kidogo hasa unapomuhusisha kiongozi wa juu wa nchi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad