NIONYESHE Demokrasia Ndani ya CHADEMA, Nami Nitakuonyesha Udikteta Ndani ya UKAWA

Na Fred Mpendazoe

Wakati Zitto Kabwe anafukuzwa ndani ya, Freeman Mbowe aliwaaminisha watanzania kuwa Zitto ni Msaliti na kwamba hastahili kushirikiana kwa lolote na msaliti. Freeman Mbowe akaendambali kwa kusema kuwa Zitto anashirikiana na
Serikali na CCM kuihujumu CHADEMA wakitoa
mfano wa Waraka wa Siri wa Zitto Kabwe.

Taarifa zipo zikionyesha kwamba Mwaka 2004, Freeman Mbowe alifanyamarekebisho ya Katiba ya CHADEMA kinyemelakwa kuondoa ukomo wa uongozi ili awe
Mwenyekiti wa kudumu, sifa mojawapo ya
kiongozi dikteta. Hadi Leo hii kila kiongozi anayetaka
kugombea uenyekiti wa CHADEMA anafukuzwa uanachama kamailivyotokea kwa ZITTO
KABWE. Yaliwakuta pia akina Kitila Mkumbo na
Samson Mwigamba. Je Mh Tundu Lissu hiyo ni demokrasia pana ?

Mchakato wa kumpata mgombea wa UKAWA hakika umeacha maswali mengi na wengiwamekuwa na majeraha yasiyopona. Ni sababuya Dr Slaa kuachia nafasi ya Katibu Mkuu CHADEMA na Prof Lipumba kuachia nafasi ya Mwenyekiti wa CUF. Hakukuwa na ushindani
wowote ndani ya CHAMA wala ndani ya UKAWA. Ni udikteta wa viongozi ndani ya Ukawa ndio uliofanya
CHADEMA kumteua Lowasa kuwa mgombea Urais tena akiwa mwanachama wa chama hicho kwa siku zisizozidi 10 tu.

Mwaka 1967 Mwl Nyerere alisema, "udikteta ni Serikali ya mtu mmoja au kukundi cha watu wachache na wao ndiyo huwa sheria. Anayepinga watakayo, basi huonyeshwa cha mtema kuni. "

Udikteta haufanywi na kiongozi wa Serikali tu. Udikteta unaweza kufanywa na mtu au kikundi cha watu nje ya Serikali.

Kuna kikundi au mtu mmoja ndani ya Chadema ambaye huamua anayotaka na akitokea mtu mwenye maoni tofauti hutwa msaliti kama ilivyotokea wakati wa kumwonyesha cha mtema kuni Mh Zitto, Mh Kitila Mkumbo, Mh Kafulila na kumpokea Mh Lowassa. Lakini hayo yote hayamkasirishiMh Lissu na haoni sababu ya kuyapigania. Ni unafiki.

Kwa nini Mh Lissu hatoi taarifa Polisi ya kufanya maandamano ya kupinga uonevu na kudai haki na demokrasia ndani ya Chadema ? Kwa nini Mh Lissu haondi boliti hiyo kwenye Ukawa na ndipo atuonyeshe fulana yake iliyoandikwa ukuta ?. Upuuzi.

Demokrasia ipi anayoidai Mh Lissu wakati demokrasia ndani ya Chadema imewashinda?

Nionyeshe demokrasia ndani ya Chadema , nami nitakuonyesha Udikteta ndani ya Ukawa.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad