Njia Tatu (3) za Kukuza Biashara ili Kupata Faida Kubwa


Uhali gani mpenzi msomaji wa makala hii ya muungwana blog? Ni matumani yangu u mzima wa afya tele na pia kama haupo vizuri kiafya basi usisajali kwa uweza wa mwenyezi  Mungu utapona na kuendeleza kulisukuma gurudumu hili la mafanikio.Katika somo letu la leo kama linavoeleza hapo juu tutaangalia ni hatua gani ambazo endapo utazifanya zinaweza kukusaidia kukuza biashara yako ambayo unaifanya au una mpango wa kuifanya. Matumaini yetu makubwa katika kufanya biashara ni kuona tunapata faida kubwa.Lakini matumini hayo hugeuka ghafla na kujikuta tunaacha kufanya biashara hii mara na kuanza biashara nyinyine huku tukiamini kufanya hivi ni kuzikwepa changamoto.

Ndugu msomaji  naomba nieleweke vizuri hapa , sina maana ya kwamba kufanya biashara nyingine na kuiacha biashara  ya mwanzo ni kosa la hasha sio kosa  ila tatizo ni kuhama na mtazamo uleule wa biashara ya mwanzo  kuutumia kwenye biashara mpya na kujikuta huupati faida kama ulivyokuwa ukitarajia hapo awali.Kuna biashara hasa hizi ndogondogo huwa tunaziona zipo vilevile siku zote.Huenda ukawa ni wewe muhusika wa biashara hiyo au kuna mtu na jamaa,ndugu au rafiki ambaye huwa unamuona akiwa katika hali hiyo,nitakochokieleza katika makala hii utaweza kumshirikisha pia.

Zifutazo ndizo hatua (3) za kukuza biashara ili kupata faida kubwa;

1. Panga malengo na mipango ya biashara.
Hili ni jambo la msingi kuweza kulizingatia.Kama wewe ni mfanyabiashara au unataka kuwa mfanya biashara unaweza ukapanga malengo na mipango ya kuweza kuiendesha biashara yako ili kuweza kupata faida kubwa zaidi. Malengo na mikakati yako lazima uyaandiike vizuri na uyatekeleze pia. Unaweza ukapanga malengo na mipango ya mauzo katika mwaka kwa mfano  unaweza kupanga kwa mieze mitatu mitatu.

Kwa mfano unafanya biashara Fulani lazima upange labda kila baada ya miezi mitatu uuze million tatu au zaidi na kama juu ya mpango na malengo usipokamilika unaweza ukafanya tathimini ni wapi ulipokesea? ili urekebishe ili miezi ijayo uweze kufikia malengo yako.Pia unaweza ukafanya taathimini  kama utakuwa umewajiri watu katika biashara yako kwa kujiuliza je wana mchango wowote katika kukuza biashara? Au wao ndo sababu ya ewe kushindwa?

Pia katika kupanga malendo na mipango juu ya biashara yako lazima upange juu ya muda wa kufanya biashara.Katika hili lazima ujiulize je biashara yako ni ya msimu? Kwa mfano wewe ni unafanya biashara ya kuuza makoti lazima ujue ni misimu ipi ni ya baridi kwani uhitaji wa wateja juu ya bidhaa hii ndio huwa wengi zaidi. Vilevile lazima upange ni jinsi gani utakavyochangamana na wateja ili kuweka mahusiano ya karibu na wateja wako.

2. Tazama ni wapi unakosea na kufanya marekebisho.
Mara nyingi changamoto katika biashara yeyote ile lazima zijitokeze.Hakuna binadamu ambaye amekamilika kokosea ni shemu ya mafanikio ya kibiashara hivyo usigope pindi changamoto zinapojitokeza,na pindi tunapokosea ndipo tunapojifunza zaidi.Inawezekana biashara yako haileti faida kutoka na wafanyakazi wako na vitu vingine jaribu kufanya uchunguzi wa kina na kuvirekebisha. Ewe mpenzi msomaji wa makala hii ili kukuza biashara ni lazima ufanye tathimini ni mipango ipi inakuletea faida katika biashara? kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuuzingatia. Kwani sio kila mipango unayopanga huleta faida.

3. Tambua namna ya kuongeza wateja.
Hii ni hatua nyingine pia ya kuzingatia.Inawezekana wewe ni mfanyabiashara mdogo au mkubwa au unatamani kuwa miongoni mwa wafanyabiashara tambua ya kwamba kuna baadhi ya biadhaa mteja akizinunua anaweza kukaa muda mrefu bila kununua tena mfano wa biashara hiyo ni magari,samani na vitu vingine. Katika hili jaribu kujenga mahusiona mazuri na wateja pia jaribu kuwa na kumbukumbu nzuri na wateja ili watakapokuja siku nyingine uweze kuwakumbuka.

Unaweza ukawa unawatumia wateja wako juu ya ujio mpya wa bidhaa,mabadiliko ya bei ili wakija kununua bidhaa wasishangae pia unaweza kuwaambia asante kuwa miongoni mwa wateja wako wazuri kwa kufanya hivi ni njia nzuri ya kuongeza wateja. Hivo kama utafanya hivi wateja hao hao ndio watakao kufanya upate wateja wapya kutokana na ukarimu na nidhamu uliyo nayo juu yao.

Pia unaweza kuongeza wateja kwa kutaangaza bidhaa yako kupitia njia mbali kama vile vyombo vya habari na mitandao mingine ya kijamii njia hii pia itafanya uongeze wateja pia. Fahamu ya kwamba kumpata mteja mpya ni kazi katika biashara yako ni ngumu hivo hakikisha mteja/wateja ulionao hauwapotezi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad