RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ‘JPM’ amesema yeye kama kiongozi mkuu wa nchi haogopi vitisho vya kufungwa ama kushtakiwa vinavyotajwa na baadhi ya wanasiasa baada ya kuwashughulikia wawekezaji wanaokiuka mikataba na kuhujumu uchumi wa nchi na badala yake ataendelea kuwatetea Watanzania wanyonge ili wapate haki yao.
JPM ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini humo.
“Hii nchi imejaa mafisadi, wamo wa CCM, Chadema, CUF, ACT, wazungu na wengine hawana chama.
“Siogopi kufungwa, kama mliniteua niwatetee, nitawatetea kwa nguvu zangu zote juu ya majizi, tumeibiwa vya kutosha, madini yetu yanachimbwa yanapelekwa nje na hatupati kitu.
“Wengine wamelipwa pesa ili kupinga tusichukue hatua dhidi ya majizi, nawaambia mimi kama rais nimejitoa kufa na kupona mpaka nihakikishe mali za Watanzania wanyonge haziibiwi na haki yao wanaipata.
“Watambue kwamba sitafungwa badala yao majizi ndiyo yatafungwa. Ilikuwa lazima tubadilishe sheria zetu hatuwezi kuendelea kuibiwa rasilimali zetu,” alisema Rais Magufuli.
RAIS Magufuli Afunguka...Siogopi Kufungwa.......
3
July 23, 2017
Tags
Maendeleo ni sawa na kama vile mtoto tangu siku ile anazaliwa mpaka anafikia umri wa kuitwa mtu mzima (yaani matured)kwa hiyo usifikiri kuwa ulipoambiwa TZ kuna gas ukafiria kuwa within a week mambo yatakuwa poa hiyo ni hatua kwa hatua mdau mpaka mambo yakamilike ili nchi na wananchi waje kufaidika na hiyo raslimali huo ni mfano wa gas na hata hizo raslimali nyingine process zake ni hivyo hivyo pia "PAPARA PAPARA ULEKE"Wahenga walisema
ReplyDeleteLakini Viongozi wetu wa ngazi za juu Tanzania ni mizigo. Hawajui kwamba aseti kubwa ya nchi hii ni Watanzania wenyewe. Elimu ya juu kwa Watanzania wote. Kunatofauti ya kutoa elimu bure ambayo ni pumba na elimu yenye manufaa. Fikra za kizamani bado ndizo zinazotuangusha. Utakuta Maraisi wetu badala ya kuwatumia Wasomi wenye uwezo wanakuwa madictator kuwaumiza, kuwadharalisha wenye uwezo wa kufukiri. Hawajui namna gani wawatumie kwa manufaa ya Watanzania. Inferiority complex ni tatizo. Mtu wa kisomo cha zamani haendani na mwamko kasi wa kidunia, bado anatumia mfumo kale ambao hauendani na mabadiliko ya sasa. Anaweza kuwa mzuri lakini bila kuelewa anachokifanya kinakwamisha Taifa zima. Hii ndo sababu ya matatizo yote haya yanayoikumba Tanzania kwa sasa. Watu hawana mwamko kuendana na wakati. Ni waoga wa kila kitu. Unakubali globalization bila kujua nani yupo numa ya hiyo globalization. Wamekaa huko, Wanawaleteeni Tanzania mnakubali kupokea harakaharaka bila kujua madhara yake na mnaiharibu nch nzima. Kwa nini mpokee matakwa yao kwa manufaa yao. Je hivi mnayayatimiza kwa misukumo ya Wawekezaji ni agenda zenu? mbona hatujaziona agena zenu mwaka mmoja, mitano, kumi , kumi na tano. Kusudi wakizileta zao muangalie je zina umuhimu au zinaendana na zenu? ndico Wapinzani walia miaka yote hii lakini maraisi wetu na chama Tawala hawalielewi hili, hawajali, ndo maana kuda haya majibishano kati ya utawala wa CCM na wapinzani. Taifa halijakaa kunyesha mfumo wote wa maendeleo ukajulikana wazi, na huu ni upotoshaji mtupu. Nawashangaa Mawaziri wote wanaotetea, Wabunge wote, na Wanaccm wote. Bunge ndich chombo cha kuhakikisha hata mambo na Bunge limetekwa . Ni wachache sana wenye werevu. Namshangaa Zitto pia. Namshangaa Lipumba, nawashangaa wale wote wenye elimu za juu Tanzania nzima mnaounga uongozi potoshi. Ni lini mtakaa na kujiuliza elimu zetu zinafaida gani kama tunashindwa kuzitumia vipasavyo, au tunanyimwa uhuru wa kuzitumia, na vielekezo, au viashirio vya damu , unyanyasaji vyote mnaviona?
ReplyDeleteHamlipendi Taifa lenu. Mamuupendi uhuru wa kufanya kazi, kufurahi bila kunyanyasiwa?
Mbona wote mnakuwa vibaraka. Sasa faida za elimu zenu ni nini? utii wa kikondoo?
ONGEA YOOOOOTE LAKINI SI AWAMU HII YA TANO.IF YOU DONT KNOW IS BETTER SHUT UP YA MOUTH..YAANI NI HIVI AWAMU HII AFAGILIWI MTU WA JINSIA ,RIKA ,CHEO CHA AINA YOYOTE,WALA CHAMA.NA WALA HAOGOPWI MTU HAPA KAZI TU..km wewe au jamaa zako walikuwa wapiga madeal na sasa wanahemea juu husiongee vitu kisiasa na kiudaku nazi,ndo mnavyo taka ninyi kubulizwa ukizingua-UFISADI,UCHOCHEZInk.kanyee debe..big up magu KAMUA BABA KAMUA mpaka maji waite mma..
ReplyDelete