Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa Marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ndio waliotengeneza maisha yake ya kisiasa hadi kuwa kiongozi.
Rais Magufuli ameyasema hayo Jumatatu hii, wilayani Chato wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation. “Nakumbuka siku hiyo tulikuja hapa Chato na wewe (Mkapa) Msafara ulisimamishwa na ukawaambia wananchi wa Chato nichagulieni huyu, nakumbuka ulikuwa umevaa viatu vyekundu,” amesema na kuongeza: “Kwa bahati nzuri, wananchi wa Chato wakanichagua, baadaye ukanichagua kuwa naibu waziri. Wewe ulinitangaza, sikustahili chochote, maneno yako yalikuwa na nguvu kwa Watanzania.” “Kwangu mimi nyinyi mlitengeneza maisha yangu katika uongozi. Pia nawashukuru sana viongozi wa awamu ya kwanza, Nyerere na Mwinyi ambao walitengeneza mazingira mazuri ndani ya Chama cha Mapinduzi. Mimi sina cha kuwalipa jukumu langu ni kuwatetea na ninawaahidi Watanzania kuwa nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote, namuomba Mungu asinifanye nikawa na kiburi namuomba asinifanye nikasahau nilipotoka.”
TOA MAONI YAKO HAPA
Tunaweza kucheka. Lakini kuna namna. Kama viongozi.
ReplyDeletePia Tujiulize ni viongozi wepi waliotusababishia haya mambo. Wako wapi na je tunawafikiriaje. Je. Hawakujua, walidanganywa, walishiriki, au walizidiwa . Mkuu wa mkoa Geita alitolewa kwa kushindwa kudhibiti kazi. je Wakuu wa nchi tunawachukuliaje?
ReplyDelete