RAIS Magufuli: Wawekezaji Wakichelewa Kufanya Mazungumzo na Serikali Nitafunga Migodi yote nchini

Akizungumza na wananchi akiwa eneo la Kakonko,Kigoma,maghiribi mwa Tanzania,Rais Magufuli ameonya kufunga migodi yote iwapo wawekezaji wataendelea kuchelewa kwa ajili ya mazungumzo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara katika wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo yupo kwa ziara ya siku tatu. Amesema haiwezekani makampuni hayo yanaendelea kuwa kimya wakati wameshakubaliana kuanzisha mazungumzo haraka.

"Makampuni ya madini yaliyoahidi kukaa na serikali kuzungumza, wafanye haraka wakiendelea kuchelewa nitafunga migodi yote wanayomiliki" Rais John Pombe Magufuli

Wakati huo huo, Wizara ya Nishati na Madini ya Tanzania imesimamisha shughuli za utoaji leseni za utafutaji na uchimbaji madini, mpaka tume ya madini itakapoundwa na kuanza kufanya kazi rasmi.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Take five mr.president kwa huo msimamo wako walizoewa kudekezwa wakati wanatuibia raslimali zetu kama vile sisi tuna shida nazo wakati wao ndiyo wahitaji kubwa wa hizi raslimali zetu wanaelewa fika kuwa bila Aftika wao ni bure kabisa ila walitufanya tuamini kuwa bila ya wao Afrika ipo mashakani kitu ambacho si kweli ila wao ndiyo wanaihitaji Afrika usiku na mchana na wakati ni huu kama alivyosemaga mzee Julius Kambarage Nyerere ikaze kamba mpaka waione chungu ya jiwe kudadeki zao hao wakoloni mamboleo Mungu akulinde mr president

    ReplyDelete
  2. Baba JPM.. NI SAWA KABISA.ANGALIA HII HAPO CHINI NI BORA KUFUNGA.
    https://youtu.be/IhYROWOayLw

    ReplyDelete
  3. Acasia na wenzenu wote milio kama akasia. Samahanini sana. Mchanga ni wetu!! na Mitambo ni yenu. The deal is Chukueni mitambo yenu au tuuzieni na sisi tunabakiki na mchanga wetu na tutaupenmbua hapa kwetu. Deali na Magumashi hatukuna tena kwa Tanzania yetu ya JPJM na sisi wananchi wakereketwa.
    Mnakaribishwa kufanya mazungumzo ya pack and Gooo!!! lakini Kuibiwa hatutaki tena na wala haito tokea!! Uchungu tunao na uwezo wa kufanya hilo tunao. Sababu pia Tunayo. Na TUNATHUBUTU kwa sasa. The leadership has focused on Development and this is part of the Tools to Achieve a NEW Era in TANZANIA. Long live JPJM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad