Ruvuma: Mashinji (Katibu Mkuu wa CHADEMA) na Wabunge Wawili, Washikiliwa na Polisi

Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe ambaye pia ni Mkiti wa Chama Kanda ya Kusini pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Mbamba Bay. Wamepelekwa kituoni kuhojiwa ambapo Katibu Mkuu Dkt. Mashinji ametakiwa kueleza kwanini yuko Mbamba Bay na aeleze amekwenda kufanya nini.

Polisi wamemkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza leo.

Tutaendelea kuwajuza.

*Makene*

Source:Jamii Forums
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Je Raisi Pombe Magufuli unaunga mkono kwa kamatakamata kwa Wapinzani. Je hii ni Amri yako. Mbona umekweda Chato na umekaa mkutano wa hadara kama mwenyekiti wa CCM hukukamatwa? Siasa chafu ndo hizi. Sijawahi kukusikia unakemea hata. Inamaana unaunga mkono? je Kwa nini kuwa na vyama vingi mkiwanyima haki wapinzani? Sijawahi kuwaona polisi wakiwashika Wanaccm hata. Je CCM tu ndo chama teule nchini?Mbona mnawadharalisha binadamu kama wanyama? Kibiti kumewashinda.Ukoloni mamboleo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad