Ukiacha mtafaruku uliojitokeza baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kusema kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba watu waliobadili jinsia hawataruhusiwa kwenye Jeshi la nchi hiyo, takwimu zimekuwa zikitolewa kuonesha kwamba watu waliobadili jinsia wanahitaji gharama ndogo sana za huduma za kiafya.
Takwimu hizi zinajaribu kulinganisha gharama ambazo Ikulu ya Marekani inatumia kila mwaka kununua dawa za kusaidia wanajeshi wenye matatizo ya kusimama kwa uume: takribani dola za Marekani milioni 84 (zaidi ya bilioni 188), kwa mujibu wa gazeti la jeshi la nchi hiyo.
Kwa upande mwingine, Shirika la Rand limekadiria kwamba huduma za kiafya zinazotokana na kubadilisha jinsia litaongeza bajeti ya jeshi la nchi hiyo kwa dola za Marekani milioni 8.4 kwa kiwango cha juu (bilioni 19).
Je, kwanini jeshi la nchi hiyo linatumia fedha nyingi kiasi hicho kununua dawa za kuongeza nguvu za kiume?
Wazee waliostaafu
kwanza, inatakiwa ieleweke kwamba taarifa hizi zinatokana na gazeti la jeshi hilo toleo la mwezi Februari mwaka 2015 liliripoti kutokana na taarifa zake za mwaka 2014 kutoka Taasisi ya Afya ya Jeshi la Marekani.
Kiasi cha dola hizo za Marekani milioni 84.2 (zaidi ya bilioni 188) kilikuwa ni matumizi ya Jeshi kwa mwaka huo, lakini pia liliripoti kwamba dola milioni 294 (zaidi ya bilioni 658) zimetumika kununua dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya Viagra, Cialis na nyinginezoza aina hiyo tangu mwaka 2011.
Gazeti hilo lilibainisha kuwa gharama hii ni sawa na kununua ndege kadhaa za kivita za kisasa kabisa.
Mwaka 2014, dozi milioni 1.18 za dawa zilitolewa na nyingi kati ya hizo ilikuwa ni ya dawa za Viagra. Lakini zilikuwa na kwa ajili ya nani? Jibu la swali hili linakwenda kuelezea matumizi makubwa kiasi hicho.
Ni kweli kwamba baadhi ya dawa za kurekebisha matatizo ya kusimama kwa uume zilikuwa zikigaiwa kwa watumishi waliopo jeshini muda huo, lakini nyingi zilikuwa zikigaiwa kwa makundi mengine, yakiwamo mamilioni ya wastaafu wa jeshi pamoja na familia zao. Kwa taarifa sahihi, watu takribani milioni 10 wanakadiriwa kuwa wanahudumiwa na mfumo wa Afya wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani uliokuwa na gharama ya dola bilioni 52 mwaka 2012.
Ni kweli kwamba baadhi ya dawa za kurekebisha matatizo ya kusimama kwa uume zilikuwa zikigaiwa kwa watumishi waliopo jeshini muda huo, lakini nyingi zilikuwa zikigaiwa kwa makundi mengine, yakiwamo mamilioni ya wastaafu wa jeshi pamoja na familia zao. Kwa taarifa sahihi, watu takribani milioni 10 wanakadiriwa kuwa wanahudumiwa na mfumo wa Afya wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani uliokuwa na gharama ya dola bilioni 52 mwaka 2012.
Inajulikana wazi kwamba matatizo ya kusimama kwa uume ni tatizo linalowakumba zaidi wazee na yawezekana ikawa ndio sababu ya gharama kubwa ya kuwahudumia wastaafu wa Jeshi la nchi hiyo.
Ki usahihi wa takwimu za nchi hiyo, gazeti hili liliripoti kuwa ni chini ya asilimia 10 ya dozi za dawa hizo ndiyo zilitolewa kwa wanajeshi waliopo kazini.
Hata hivyo, idadi ya wanajeshi wenye matizo ya upungufu wa nguvu za kiume kwa wanajeshi walio kazini kwenye Jeshi la Marekani imekuwa ikiongezeka tangu kipindi cha kuanza kwa vita za Iraq na Afghanistan.
Sababu za kisaikolojia
Utafiti wa mwaka 2014 uliofanywa na Taasisi ya Afya ya Jeshi la Marekani (AFHSB) ulionesha kwamba wanajeshi 100,248 wenye matatizo ya kusimama kwa uume walipatikana katika wanajeshi walio kazini kati ya mwaka 2004 na 2013, ikiwa idadi ya wanajeshi wenye matatizo hayo kwa mwaka ikiwa imeongezeka kwa zaidi ya mara mbili katika kipindi hicho.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, karibia nusu ya waliripoti shida hii ni kutokana na sababu za kisaikolojia.
Matokeo ya utafiti yaliyochapishwa mwaka 2015 kwenye Jarida la Tiba ya Mapenzi yalibainisha kwamba wastaafu wa Jeshi hilo wenye msongo wa mawazo uliotokea baada ya matukio makubwa walikuwa kwenye nafasi kubwa sana ya kupata tatizo hilo kuliko kwa wastaafu wenzao ambao hawakuwa wanajeshi.
Utafiti mwingine ulionesha kuwa asilimia 85 ya wanajeshi wastaafu wanaume waliowahi kwenda vitani wameripoti kuwa na matatizo ya kusimama kwa uume ambayo ni karibu mara nne ya idadi ya wale waliorudi kutoka vitani na wakawa hawana tatizo la matatizo ya kisaikolojia.
Mwaka 2008, Shirika la Rand liliripoti kwamba kila mwanajeshi mstaafu mmoja wa kati ya wanajeshi wastaafu watano wa Jeshi la Marekani waliowahi kushiriki vita vya Iraq na Afghanistan walikuwa wanasumbuliwa na matatizo ya kiakili na kisaikolojia ikiwemo msongo mkubwa wa mawazo.
Hata hivyo, takwimu za hivi karibuni zinazohusu uchunguzi uliofanywa kwa wanajeshi walio kazini kati ya mwaka 2004 na 2013 ambazo zinadaiwa kufichwa kwenye makabati ya Idara ya Ulinzi kitengo cha Afya ya wanajeshi zinaeleza kwamba inabidi kuwa makini kujaribu kutengeneza uhusiano kati ya vita ambazo nchi hiyo ilipigana hivi karibuni, msongo wa mawazo na matatizo ya kusimama kwa uume na jeshi la nchi hiyo kutumia fedha nyingi kununua dawa za Viagra.
Hii ni kwa sababu inadaiwa kuwa wanajeshi ambao hawakuwahi kupelekwa vitani ndio wapo kwenye hatari kubwa ya kupata tatizo hili kuliko wenzao ambao wamewahi kwenda vitani.
Matatizo ya kusimama kwa uume huwa yanahusishwa na magonjwa kadhaa ya binadamu yakiwamo magonjwa ya moyo, shinikizo la juu la damu na kisukari.