SAID Aliyetobolewa Macho na Scorpion Amgeuzia Kibao Mkewe

Songombingo la ndoa ya jamaa aliyetobolewa macho na Scorpion, Said Mrisho na mkewe Stara Sudi ‘Mama D’ juzikati lilichukua sura mpya baada ya Said kumgeuzia kibao mkewe na kusema watoto mapacha waliozaliwa na mwanamke huyo anahisi siyo damu yake.

Awali akizungumza na kituo kimoja cha redio jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Mama D alisema kuwa mumewe huyo aliwahi kukana mimba ya watoto hao lakini Said aliyekuwepo redioni hapo alikanusha na kusema kuwa, jamii ijue kuwa watoto ni wake hivyo akampa mkewe matumaini mapya.

Hata hivyo, Jumanne iliyopita Ijumaa liliibuka nyumbani kwa Said, Vingunguti jijini Dar anakoishi na yule mkewe Mwarabu na katika maelezo yake akasema, kauli yake kutoka moyoni ni kwamba anahisi wale watoto mapacha siyo wake.

“Jamani iko hivi, kabla sijapata ulemavu nilikuwa na miezi kama mitatu sijakutana na mke wangu, baada ya kupata matatizo nikawa na miezi mingine mitatu bila kukutana kimwili, baada ya kuishi kwa siku nyingi bila kukutana, siku tulipokutana tu wiki chache baadaye akaniambia ana mimba ya miezi minne!

“Ndiyo maana nasema nina wasiwasi na hawa watoto mapacha si wanangu. Haya yote sikutaka kuyasema tangu mwanzo kwa kuwa sikutaka mvutano na mwanamke huyo, wala sikuona kama ni vema kusema maovu yake mengi,” alisema Said.

Baada ya maelezo hayo, paparazi wetu alimvutia waya Mama D ambapo baada ya kumwagiwa maelezo ya Said alitokwa na povu ‘si la nchi hii’ huku akimuomba Mungu ampe mabalaa mzazi mwenzake huyo.

“Mungu amlaani maisha yake yote na niseme tu, natamani apate balaa kubwa kuliko hilo alilonalo, naona ulemavu umemfanya akili yake ishindwe kufikiri sawasawa.

“Ambacho naweza kusema ni kwamba, kama ana wasiwasi na hawa watoto anaweza kwenda kupima DNA akikuta watoto si wake, ruksa aniache nao, nitawalea peke yangu na kama vipimo vitaonyesha watoto ni wake naapa kwa jina la Mungu naenda kumtelekezea vichanga hivi mlangoni kwake awalee mwenyewe,” alisema mama D.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe baba we ugopa Mungu huo mtihani uliopewa bado nini unataka? unamdhalilisha mama ya watoto wako hivo ukae ukijua malipi ni hapa dunia na kwa yalio kupata alisimama na wewe sasa umemgeuka kama ambae humjui kabisa rudi kwa mola wako uombr msamaha na umuombe msamaha mama watoto wako kabla kipigo cha Mwenyezi Mungu hakijakufika omba toba sio vizuri hivo basi umepata kidogo ujitutumue hivo hadi kumkana mwenzako

    ReplyDelete
  2. tabia ya Saidi sio nzuri. kashapata pesa za msaada sasa anamgeukia Mama D. ila akumbuke alivyosaidiwa wakati katolewa macho.

    ReplyDelete
  3. WE DOGO SAID,KWA HILI NAWASIWASI WATOTO HAO NI SAID,MPAKA MTU YUKO TAYARI KWENDA KUPIMA DNA AAH NO WHAT MEANS ANAUHAKIKA NA ANACHOKISEMA HAROPOI,COSE NDA HAIONGOPI INAUMBUA,DAWA YAKE NI:-MALI ALIZOCHANGISHWA MPAKA KUVIMBISHWA MAKALIO SASA ZIGAWANYWE KWA MBILI,HALAFU YEYE SAID AENDE HUKO KWA MWARABU,MWACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO,CHEZEA WAARABU WEWE HAWAJAZOEWEA SHIDA MWACHE ZIKIISHA HIZO ATASEPA...MWACHE MUNGU ANAMUONA..NB:kapime DNA NA WATOTO..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad