Sakata la Simba Kumnyima Kibali cha Kuondoka Mchezaji Abdi Banda Lafika Pabaya....Simba Wadai Hawafanyi Kazi Kwa Shinikizo la Mtu

Klabu ya Simba inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya mchezaji Abdi Banda ambae alilalalamika jana kupitia vyombo vya habari,kuwa klabu imemkatalia kumpa barua ya kumuacha (REALESE LETTER) ilhali yeye amepata Timu huko Afrika kusini na huku akiwa amemaliza mkataba wake.

Ni kweli Banda amemaliza Mkataba na klabu, na jana alikuja ofisini kwetu kutaka barua hiyo, lakini akakumbushwa kuwa,ukiwa umemaliza Mkataba haupaswi kupewa barua hiyo,wanaoandikiwa barua hiyo ni waajiriwa ambao bado wana mikataba na labda kwa sababu yoyote ile,klabu inaamua kuachana nao.

Lakini kwa kuwa Banda aliitaka hyo barua, akaambiwe aandike barua fupi tu ya kuomba Realese Letter, ili ibaki kumbukumbu kwa klabu, lakini kwa mshangao wa maafisa wa klabu aligoma kuiandikia barua klabu na kuamua kukimbilia kwenye vyombo vya habari na Blogs.

Klabu imesikitishwa sana na kitendo hicho kinachojirudia cha kutafuta huruma kupitia Media,huku akijua kuwa anaikosea heshima klabu na kuipaka matope bila sababu.

Simba inaamini sana utamaduni wake wa miaka mingi wa kuwaruhusu wachezaji wake kwenda nje ya nchi kucheza soka, pindi wapatapo nafasi hiyo,lakini inasisitiza sana suala la utaratibu,haijawahi kutokea kokote duniani,mchezaji aliyemaliza mkataba kudai Realise letter,na kiukweli tumeshangazwa pia na baadhi ya vyombo vya habari kulishupalia jambo hili bila hata kutusikiliza (kubalance story).

Na kwa kupitia barua hii, klabu inawaambia haitafanya kazi kwa shinikizo la mtu au chombo chochote kile huku tukifahamu ni kinyume na utaratibu na utamaduni wa mchezo huu unaopendwa duniani kote

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad