SHAFFI Dauda Akiri Kufanyiwa Mchezo Mchafu

Siku ya Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU baadhi ya wadau wa soka wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).



Miongoni mwa hao ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Dar es Salaam (DRFA) Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza.

Mara baada ya tukio hilo kupita, Shaffi Dauda akiri kuhojiwa na TAKUKURU Mwanza, asema alikuwa katika vikao vya maandalizi ya Ndondo Cup na si vikao vya uchaguzi.

Kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra kinachorushwa na radio Clouds Fm Dauda amesema.
“Kwenda jioni na Mkazuzu kwenda kuangalia “logistics” za Vila Park, Press tufanyie sehemu gani kesho. Tunafika pale tumeyamaliza tunamtafuta Rama hata Rama sijaonana nae maskini” amesema Dauda.

Shaffi Dauda ameongeza kwa kusema kuwa “Tumekaa tunakula chakula mara wazee hao wamevamia dakika tano hazikufika kulikoni ?, eeh mnafanya nini ?, difenda na takukuru. Kumbe siasa za mpira zimeanza mambo ya uchaguzi”.

“Kumbe sisi tunakuja huku Mwanjala anaambiwa usiende huko Mwanza kunawatu walikuwa washapanga mipango yao huku ambao wao wanafikiri kuongoza mpira wanchi hii ndiyo wenye haki miaka yote wameshakuwa viongozi lakini sasa hawapo kwenye mfumo wanalazimisha kuwemo”. Na sisi kwa sababu zimeshakuja mamlaka unakuwa mpole tumewasilikiza tukaenda tukaojiwa maelezo tukawapa mpaka saa tisa baada ya hapo tukaruhusiwa tumetoka kwa dhamana lakini ni siasa za uchaguzi”.

“Kumbe tumekaa pale kunamtu anamtumia mtu meseji ebwana toka hapo sasa hivi kunakuja TAKUKURU maskini simu ilikuwa Silence watu hawajui lakini nashukuru Serikali imefanya kazi yake”.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad