TABIA Mpya Inayokera Mjini ya Wanawake Kujipiga Picha Ovyo Ovyo.......

Aisee hii tabia inanikera sana, tabia ya kupiga piga picha kila wakati wahanga wa kubwa wa hii tabia ni wanawake, unaenda na mtu sehemu  ile mmefika tu unaona mdada ametoa kasimu kake anaanza kupiga picha, sio kama anapiga picha moja, atapiga picha kama 20 katika eneo moja na wakati huo huo.

Huwa najiuliza hii mipicha yote huwa mnafanyia kazi gani? Wengine kila wakati wa kula wanapiga picha, kwenye simu kuna mapicha ya aina moja kibao hii tabia mwanzoni alikuwa nayo girl wangu ameacha baada ya kumchana kuwa hizo mambo sizizimikii, sasa imebaki kwa watu ambao nafanya nao kazi na watu wangu wa karibu mpaka imekuwa kero, wakiwa ofisini picha, wakienda kula picha. Napataga hasira natamani nichukue visimu vyao nivitupilie mbali.

Kama una tabia hii acha mara moja haipendezi kabisa, au kama unapiga picha piga moja au mbili inatosha sio unapiga picha kama 20 mpaka unasahau kilichokuleta, inakera sana!
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Masikini akipata na matako hulia mbwata

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad