TANZIA...Jaji Ambaye Rais Magufuli Aliridhia Ombi Lake la Kujiuzulu Afariki Dunia


Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu  hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga

Amesema marehemu ameacha watoto wanne.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad