Tundu Lissu Afunguka...Adai Serikali Ina Mkakati wa Kuminya Uhuru wa TLS ili Kuwadhibiti Wanasheria..

Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kimekutana kujadili na kutoa msimamo wao juu ya mapendekezo ya Serikali kuanzisha Bodi ya Usajili wa Mawakili huku kikiwataka mawakili wake kusimamia maadili ya taaluma yao ili kutimiza majukumu kwa haki.

Akizumza kwenye mkutano huo Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria kwa ujumla iwapo siasa itaingia kwenye kazi zao sheria.
Amesema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria kadri itakavyoona inafaa.

"Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa Huo ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria kuingia kwenye siasa, jambo ambalo  linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa sababu matokeo yake ni mabaya" alisema Mh. Tundu Lissu.

Mbali na hayo Lissu amewaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa kusimamia taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa na maana ya  kuwepo kwa chama hicho.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi jamani hata wanash
    wanasheria wa Tanganyika waliomchagua Lissu kuwa raisi wa TLC wanahitaji kutahiniwa kwani wana kasoro
    Naomba Magu aitishe uchaguzi kama Theresa May wa UK tuone hao vichwa vya dagaa watarudi wangapi mjengoni hasa huyu anakera sana sana
    Tafuteni namna ya kumfanya asisikike tena na siasa zake labda huko Singida walikomchagua wanamuihitaji lakini siyo Tanzania

    ReplyDelete
  2. Dagaa ni wewe mwenyewe usiyejitambua ni dagaa. Na hii inatokana na ujinga usiofundishika. Inamaana hakuna chance ya kufunguka hata. kuna jiwe machoni, mdomoni na kibanzi masikioni. Ndo maana kwa miaka takkribani CCM imeua na kuiangamiza nchi nchi .kisa Ujinga wa wengi kama wewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad